Zari Amkuwadia Dogo wa Diamond kwa Mrembo Huddah Monroe
Mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ anadaiwa kumkuwadia dogo anayeishi na kufanya kazi ya muziki na Diamond, Rajabu Abdulkhali ‘Harmonize’ kwa mrembo maarufu Afrika anayeishi Kenya, Huddah Monroe.
Chanzo chetu kilicho karibu na mastaa hao kilitutonya kuwa, Zari na Huddah walikuwa nchini Kenya ambapo Diamond akiwa na Harmonize walitua huko kwa mambo yao ya kisanii.
“Harmonize na Diamond walipotua airport, Zari na Huddah ndiyo waliowapokea. Wakawachukua mpaka hotelini.
“Walipofika, baba na mama Tiffah wakawa bize na yao, hapo ndipo Zari alipomchombeza Huddah ajiweke kwa Harmonize. Si unajua tena Huddah naye hajatulia, hakukataa na ndipo dogo akajichukulia mzigo na kwenda nao chumba kingine,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kudai kuwa, walichokifanya huko wanakijua wenyewe ila walipigana picha na kurekodiana video zikiwaonesha kimahaba.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, Ijumaa lilifanikiwa kunasa baadhi ya picha zikimuonesha Huddah na Harmonize wakiwa ‘romantic’ ikiwa ni pamoja na clipu ikiwaonesha wakishikana na kuchezeana kimalovee.
Harmonize atafutwa
Jitihada za kumpata Harmonize zilifanyika kupitia simu yake ya mkononi na alipopatikana alisema ni kweli alipokuwa Kenya alifanikiwa kukutana na Huddah, akakiri kuwa aliyewaunganisha ni Zari.
“Unajua mimi sikuwa nikimjua Huddah, nilikuwa nikimuona kwenye TV na magazeti tu. Sasa tukiwa kule Zari aliponiona niko mpwekempweke, ndiyo akaniweka pale, mambo mengine ni siri yetu bwana,” alisema dogo huyo anayefanya vizuri kwenye muziki.
harmonizeHuddah ni nani?
Ni modo anayefanya shughuli zake nchini Kenya lakini amekuwa akishaini Afrika kutokana na skendo zake za kupiga picha za utupu.
Mrembo huyo aliwahi kuingia kwenye bifu zito na Mtangazaji wa Clouds, Loveness Malinzi ‘Diva’ chanzo kikiwa ni Mwanamuziki Jackson Makini ‘Prezzo’ aliyekuwa mpenzi wa Huddah lakini akachepukia kwa Diva.
from Blogger http://ift.tt/1NM0cyy
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment