Wanasayansi wanasema: Kama mwanamke anatabia hizi 5, Usimwache

Wanasayansi wanasema: Kama mwanamke anatabia hizi 5, Usimwache
Watu katika mahusiano yaliyodumu muda mrefu lazima kila mmoja atajiuliza huyu ndiye mtu ambaye nataka kuishi nae maisha yangu yote? Mwanamke huyu naye ishi naye ndiye chaguo sahihi?
Wanasayansi duniani kote wanafanyia utafiti masuala magumu katika mahusiano na mapenzi sikufichi wametumia maelfu ya masaa kufikiria ni jinsi gani watu watafaana na mambo gani wanaitaji kufanya katika maisha yao ili kuleta furaha na kudumisha mahusiano yao.
leo tumejaribu kukuletea mambo muhimu ambayo yamefanyiwa utafiti na wanasayansi hao juu ya kudumisha mahusiano. Kama mwanamke unayeishi naye anatabia na matendo haya 14 fahamu umempata mwenyewe.
1. Awe na akili kuliko wewe
Unapoangalia mwanamke wa kuishi naye katika maisha yako yote, hakikisha awe na akili.
Profesa Lawrence Whalley, kutoka chuo cha Aberdeen amekuwa akifanyia utafiti suala la dementia ambapo mtu anakuwa anapoteza kumbukumbu, na akili zake kuwa kama mtoto mara nyingi tatizo hili huwatokea wazee kwa hiyo profesa huyo anasema ukimpata mwanamke mwenye akili anaweza kukusaidia baadae uzeeni unapokumbwa na gonjwa hilo la uzeeni. Profesa huyo alitoa ushauri wake anasema kwamba: “Kitu ambacho mwanaume hafahamu kama anataka kuishi maisha marefu – anatakiwa kuoa mwanamke mwenye akili hakuna msaada mkubwa wa baadae kama kuoa mwanamke mwenye akili.” alisema profesa huyo.

2. Anacheka unapomchekesha

Ni kweli unahitaji mwanamke ambaye anacheka kila unapomchekesha. Katika utafiti uliofanywa
na mwanasaikolojia kutoka chuo cha Westfield State anashauri kwamba kuwa na mtu ambaye unamfurahisha ni muhimu kwa mwanaume kuliko mwanamke. Kama unamtu ambaye mnafurahi kwa pamoja, huyo ndiye sahihi wakuishi naye.
3. Muwazi
Kuwa na mtu ambaye ni muwazi katika jamii na anayeweza kuongea na watu wengine ni jambo zuri katika mahusiano.
Utafiti uliofanywa na chuo cha Westminister unasema kwamba watu ambao wapo wazi na wanaweka mambo yao wazi wanavutia zaidi. Muandishi wa utafiti huo alisema kuwa wazi ni muhimu kwa sababu watu watakufahamu zaidi kutokana na tabia za wazi ulizonazo.
4. Anatoa msaada katika mambo yako
Kwa kipindi kirefu wanasayansi wamejaribu kuweka bayana kwamba wanaume wanapenda kuoa wanawake wasio jiweza. Katika kitabu kilicho andikwa na Christine C. Whelan “Why smart men marry smart women”, anaonesha kwamba wanawake ambao wamesoma na uwezo mkubwa hawaoi watu wasioendana nao.
Kumbuka kuwa na mwanamke ambaye anajiweza atakusaidia kufikia ndoto zako na kamwe hato kutegemea. Wewe hauhitaji kuhofia juu yake kwa sababu kila kitu yeye anajigharamia mwenyewe.
5. Anauhusiano mzuri na wazazi wake
Kama unataka kujua mtu wako atakuwaje baada ya miaka 30, angalia jinsi anavyoishi na wazazi wake sasa ndipo utajua ataishi vipi na wewe ndani ya miaka 30.
Watafiti kutoka chuo cha Alberta waliwauliza maswali watu 2970 walika zote na kupata majibu juu ya muenendo wa mahusiano yao kutokana na vile walivyokuwa wakiishi na wazazi wao.
Ila hii haimaanishi kwamba mahusiano na wazazi wake lazima yawe mazuri. “Mahusiano mazuri na wazazi wako ndiyo mchango mzuri wa jinsi gani utakavyokuwa ukiishi na mwenza wako kitabia – kama ni mbaya au nzuri – katika mahusiano ya karibu,” Muandishi Matt Johnson aliandika katika kitabu chake. Njia pekee ya kujifunza jinsi ya kuishi vizuri katika mahusiano ni kuwa muangalifu na tabia zako.
Kama utakuwa umempata mwanamke mwenye tabia hizo zote, ishi nae vizuri na kamwe usije ukamwacha. Utafurahia maisha yako kwa kuwa naye kama walivyotuelezea wataalamu hao kutoka vyuo vikuu mbali mbali.

from Blogger http://ift.tt/2lqnRf4
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment