
BUNGE
Maalum la Katiba limepitisha marekebisho ya Kanuni ili kuliwezesha
kufikia hatua ya mwisho ya upigaji kura kuanzia tarehe 29 Septemba hadi
tarehe 2 Oktoba mwaka huu. Hatua hiyo ililenga kumaliza vikao vya Bunge
hilo kwa muda uliopangwa kwa mujibu wa Sheria wa tarehe 4 Oktoba mwaka
huu. Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,
Mhe. Samuel Sitta wakati alipokuwa akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu
uwasilishwaji wa azimio la kupitisha Marekebisho ya Kanuni za Bunge
hilo. Mhe. Sitta amesema kuwa inakadiriwa kuwa wajumbe wasiopungua 480
wanatarajiwa kupiga kura na kutokana na kanuni zilivyokuwa kabla ya
mapendekezo ya mabadiliko hayo ingechukuwa siku nyingi kukamilisha zoezi
la upigaji kura kwa kupitia kifungu kwa kifungu. “Kanuni zilivyo hivi
sasa kama hatutafanya mabadiliko itachukua kwa wastani wa dakika kama
mbili kwa kila mjumbe kupiga kura kwa kila kifungu ambapo kwa siku
tutamia wastani wa dakika 960 kwa ibara moja, tunatarajia ibara zitakuwa
300…ameongeza kwa ibara hizo tungehitaji siku 300 kukamilisha zoezi
hilo ambao muda huo utakuwa kinyume na utaratibu uliopangwa tutakuwa
tunamaliza ibara moja kwa siku moja”, alisema Sitta.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment