Mkutano wa mabadiliko ya hewa waanza hii leo Marekani

Mkutano mkubwa wa viongozi duniani kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unafunguliwa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, huku kukiwa na wito wa kupunguza hali ya joto duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ndiye mwenyeji wa mkutano huo atakayewaongoza viongozi takriban 120, huu ukiwa mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu tokea ule
Image result for hali ya hewa Pix
uliofanyika Copenhagen mwaka wa 2009
 na kumalizika  bila ya mafikiano. Wanadiplomasia na wanaharakati wa mabadiliko ya tabia nchi wanauona mkutano huu kuwa  muhimu na kuelekea mkutano mwengine uliopangwa kufanyika mjini Paris mwishoni mwa mwaka wa 2015 ambao unatarajiwa kuweka mipango ya kupunguza utoaji wa gesi chafu inayoharibu mazingira,baada ya mwaka 2020.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment