Vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Pakistan ,Islamabad vimewaondoa waandamanaji kutoka makao makuu ya runinga ya kitaifa PTV.
Kituo hicho kwa sasa kimeanza kurusha matangazo
hewani baada ya kulazimishwa kusitisha matangazo hayo wakati
waandamanaji wanaopinga serikali walipovamia jengo hilo.Kumekuwa na ghasia kati ya waandamanaji na polisi nje ya majengo ya bunge.
Waandamanaji wanamtaka waziri mkuu Nawaz Sharrif ajiuzulu.
Ghasia zilizuka siku ya Jumamosi baada ya maandamanao ya amani ya takriban wiki mbili.
Picha za Runinga zilionyesha waandamanaji wakivamia vituo vya kurekodia na kuvunja vifaa.
Wanajeshi wa Pakistan baadaye waliwasili na kulidhibiti jumba hilo.
Waandamanaji hao waliwakaribisha wanajeshi hao kwa kuimba nyimbo za kuwasifu.
Kituo hicho sasa kimeanza kurusha matangazo yake lakini kisa hicho ni dhihirisho kwamba iwapo tatizo hilo halitatatuliwa kwa amani huenda hali ikawa mbaya zaidi.
Waziri mkuu Nawaz sharrif amefanya mkutano na mkuu wa majeshi Jenerali Raheel Sharif ili kujadiliana kuhusu hatua wanazoweza kuchukua.
0 maoni:
Post a Comment