Wasaniii
walioshiriki tamasha la Fiesta 2014 wakiwa na mishumaa jukwaani
wakisambaza upendo na kuwafariji wale wote waliopotelewa na ndugu
zao,waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea hivi karibuni wilayani
Butiama mkoani Mara,ambapo watu zaidi ya 40 walipoteza maisha na wengine
kujeruhiwa vibaya.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa musoma wakiwa ndani ya uwanja wa
Karume,wakati tamasha la Fiesta 2014,likiendelea huku shangwe za hapa na
pale zikiwa zimetawala kila kona ya uwanja.
Mmoja
wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Barnaba ambaye kwa sasa
anatamba na wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la Waharade akiwaimbisha
wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la
fiesta 2014
Mmoja
wa wasanii kutoka kundi la Weusi ,Nick wa Pili akiwarusha wakazi wa mji
wa Musoma usiku huu kwenye tamasha la Fiesta 2014,lililofanyika ndani
ya uwanja wa Karume.
Sehemu ya wakazi wa Musoma waliojitokeza kwenye tamasha la Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume.
Mwanadada machachari awapo jukwaani,Shilole akiimba kwa madaha kabisa
kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Pichani
kati ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael akiwa sambamba na
madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta vilivyo usiku huu ndani ya
uwanja wa Karume mjini Musoma
Mashabiki wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa na wasanii mbalimbali jukwaani usiku huu
Mmoja wa wasanii anaeokuja juu katika anga ya muziki wa hip hop,Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani.
Wakazi wa Musoma walivyojitokeza kwenye tamasha la Fiesta 2014 katika uwanja wa Karume usiku huu.
Jicho
la samaki likiwa limewakusanya pamoja mashabiki wa tamasha la Fiesta
lililokuwa likiendelea ndani ya uwanja wa Karume,mjini Musoma.
0 maoni:
Post a Comment