Erdogan:Mji wa Kobane wakaribia kutekwa

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya leo mji wa Kobane mpakani na Syria unakaribia kuanguka mikononi mwa wapiganaji wa jihadi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu akisema harakati ya ardhini inahitajika kuwashinda wanamgambo hao. Akizungumza wakati wa hotuba yake aliyoitoa katika mji wa mashariki wa Gaziantep, Erdogan amesema ugaidi hautakoma mpaka kuwepo ushirikiano wa harakati ya ardhini dhidi ya wapiganaji hao. Wapiganaji wa Kikurdi wakiungwa mkono na mashambulizi ya kutokea angani ya Marekani wamepambana vikali leo na wapiganaji wa Dola la Kiislamu kwenye makabiliano ya barabarani. Shirika la haki za binadamu la Syria limesema watu takriban 142, zaidi ya nusu wakiwa wapiganaji wa jihadi wameuwawa katika mji wa Kobane na viunga vyake tangu katikati ya mwezi uliopita.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment