Kesi ya Uhuru M Kenyatta njia panda kwa ICC.



 
 
Hague, Uhollanzi - 08/10/2014. Mwanasheria anaye mtete Uhuru M Kenyatta, ameiomba mahakama kutupilia mbali kesi inayo mkabili mteja wake, kwani haina ushahidi wakutosha.
 
Uhuru M Kenyatta ambaye anashitakiwa kwa kuhusika kwa njia moja au nyingine katika vurugu ambazo zilisababisha mauaji ya watu wasiopungua 1000 na mali nyingi kuharibiwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2007 nchini Kenya.
 
Steven Key, mwanasheria anaye mtete Uhuru M Kenyatta alisema " hii kesi in kesi ambayo haina ukweli na kila ukweli unapo ulizwa umekuwa hauwekwi mbele ya makahama."
 
" Nahivyo naiomba mahakama kuifuta kesi hii, kwani mpaka sasa upande wa mashitaka hauna cha kuonyesha kama ushahidi,na wamekubali hilo mbele ya mahakama."
 
Uhuru M Kenyatta alihudhurua kwenye kesi hiyo kama Uhuru Kenyatta, na siyo kama rais wa Kenya, baada ya kukabidhi wadhifa wa Urais wa Kenya kwa makamu wake William Ruto.
 
Kuhudhuria kwa Kenyatta katika kesi hiyo, kumekuwa ni kwa aina yake, kwani amekuwa ni mtu wa kwanza kuhudhuria akiwa kama rais aliyechaguliwa kuiogoza nchi, na kuamua kukabidhi madaraka yake kwa makamu wake na kwenda kwenye mahakama kama raia wa kawaida
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment