Mkurugenzi Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dk. Mzee Mndewa,
akisalimia na Mtoto aliyeandaliwa kwa ajili ya kukamata mkasi ya
Uzinduzi wa Kituo cha Posta Tunguu Zanzibar kwa ajili ya Wananchi wa
Mkoa wa Kusini Unguja kutowa huduma za Posta uzinduzi huo umefanyika leo
huku tunguu. kushoto Meneja Makaazi Zanzibar Bi Mwanaisha Said Ali na
Afisa wa EMS Bi Mwanaisha Said Ali na Afisa wa EMS Bi Mashhavu Mmanga,
wakishuhudia tukio hilo la uzinduzi wa kituo hicho tunguu.
Mkurugenzi Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Dk. Mzee Mndewa,akikata utepe kuashiria kukizindua kituo kipya
cha Posta Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, kituo hicho kitatoa
huduma za kiposta kwa Wananchi wa Mkoa huo, na jirani zake.
Posta Master wa Posta Tunguu Ndg Mohammed, akitowa huduma ya kuipima
barua baada ya uzinduzi wa Posta hiyi huko Tunguu Zanzibar Mkoa wa
Kusini Unguja.

Afisa wa Kitengo cha huduma za EMS Zanzibar Bi, Mashavu Mmanga akitowa
maelezo ya jengo jipya la Posta Tunguu wakati wa ufunguzi wake kwa ajili
ya Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja kuwa karibu na huduma za posta
kuwawezesha kutuma na kupokea barua na vifurushi bila ya kufika mjini
kufuata huduma hiyo.
Waheshimiwa wakimsikiliza Afisa wa Kitengo cha huduma za EMS, Bi Mashavu
Mmanga akitowa maelezo ya kituo hicho kwa mgeni rasmin Mkurugenzi wa
Miundombinu na Mawasiliano Dk. Mzee Mndewa mwenye shati la
maremborembo,
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika piocha ya pamoja
nje ya jengo lao la Posta Tunguu baada ya kuzinduliwa leo







0 maoni:
Post a Comment