Afisa
Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw. Farough Baghozah (wapili
kushoto)akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 13 Mratibu wa Mbio za Rock
City Marathon 2014, Bw. Mathew Kasonta (wa kwanza kulia) wakati wa
hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo
zitafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi
huu. Wakishuhudia wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group
Bi. Pamela Mandari, na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo
Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto).
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw. Farough Baghozah (wapili
kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kukabidhi
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni hiyo
kudhamini mbio za Rock City Marathon 2014 zitakazofanyika mkoani Mwanza
katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 Mwezi huu. Wakishuhudia kulia ni
Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi. Pamela Mandari, Mratibu wa
mbio hizo, Bw. Mathew Kasonta (wapili kushoto) na Afisa Uhusiano na
Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto).
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew Kasonta, (wa pili kushoto)
akiongea na waandishi muda mfupi kaba ya kupokea hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 13 iliyotolewa na kampuni ya TSN Group kuoitia kinywaji
chake cha Chili Willy kama udhamini wa mbio hizo kwa mwaka huu
zitakazofanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26
Mwezi huu. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TSN group, Bw.
Farough Baghozah akifuatiwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa TSN Group Bi.
Pamela Mandari, na kushoto ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni
hiyo Bi. Koiya Kibanga (wa kwanza kushoto).
====== ======= =========
Ukurasa
mpya umefunguliwa katika mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ambapo
kwa mara ya kwanza tangu mbio hizo zilipoanzishwa miaka mitano
iliyopita, mbio fupi sasa zitakuwepo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 13 kwa waratibu
wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI), Afisa
Mtendaji Mkuu wa TSN Group Bw. Farough Baghozah aliipongeza hatua hiyo,
na kusema kuwa kampuni yake inaungana na wadhamini wengine kuunga mkono
tukio hilo la kila mwaka sababu ya dhamira yake ya kuibua na kukuza
vipaji vya vijana katika riadha na kukuza utalii wa ndani kupitia
michezo.
“Tunayofuraha
kuidhamini mashindano ya mwaka huu ambayo sasa yatajumuisha na vijana
wadogo ambao wana vipaji vya kukimbia mbio fupi fupi. Hii itawapa vijana
wengi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, ambavyo vinaweza kuwa ndiyo fani
zao hapo mbeleni,” alisema Bw. Baghozah.
Alisema
kuwa kampuni yake imekuwa ikiunga mkono jitihada mbali mbali
zinazolenga kukuza sekta ya michezo na burudani nchini Tanzania, ambayo
imekuwa ikitengeneza fursa za ajira miongoni mwa vijana walio wengi
nchini.
“Hivi
karibuni tu, TSN Group iliweza kuwaleta wachezaji wa timu ya Real
Madrid ili kucheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania wa mpira wa miguu.
Hii ililenga katika kuwatia morari wachezaji wetu na vijana kupenda
michezo, wakiendelea kuongeza jitihada ili kufanikiwa zaidi katika kile
wanachofanya,” alisema.
Naye
mratibu wa tukio hilo, Bw. Mathew Kasonta alisema udhamini huo kutoka
TSN Group utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mbio hizo za Rock City
Marathon 2014, ambapo vipaji katika mchezo wa riadha vitagundulika
pamoja na kuyafanya mashindano hayo kuwa chanzo kikubwa zaidi ya
kutangaza maeneo mbali mbali ya utalii katika kanda ya ziwa.
“Baada
ya kupata udhamini toka kwa wadhamini wetu, kamati ya maandilizi ilikaa
na kukubaliana kuwa mbio za Rock City za mwaka huu zitajumuisha mbio
fupi. Hizi zitajumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale
waliopo shule za msingi madarasa ya juu. Uamuzi huo ulichukuliwa baada
ya kuona kuwa mashindano ya marathon nyingi nchini, hayana mbio fupi
ambazo zina vipaji vingi pia,” alisema Kasonta.
Alisema
mbio hizo fupi zitakuwa ni; kilomita 100, kilomita 400 na kilomita
1500. Mbio hizo zitafanyika baada ya mbio ndefu ya nusu marathoni. Bw.
Kasonta alisema fomu za usajili zinapatikana katika ofisi za kampuni ya
Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya tatu
jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi
zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza, Uwanja wa
Nyamagana na pia zinapatikana katika mtandao wa www.therockcitymarathon. blogspot.com.
“Meya
wa jiji la Mwanza, Bw. Stanslaus Mabula alifungua usajili kwa kuwa
mshiriki wa kwanza kujisajili katika mbio za Rock City Marathon 2014
ambazo zitaanza katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 26 mwezi Oktoba
mwaka huu, ambapo ataonyesha uwezo wake katika riadha kwenye mbio za
kilometa 5,” alisema.
Bw.
Kasonta aliwataja wadhamini waliyofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake
cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania,
New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group, Continental
decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB).



0 maoni:
Post a Comment