VODACOM YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SIMU DOKTA LEO
Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Dk. Sulende
Kubhoja.
KAMPUNI
ya mawasilianao ya Vodacom Tanzania imezindua huduma mpya
itakayowawezesha watumiaji wa mtandao wa kampuni hiyo kupata taarifa
muhimu kuhusu afya kwa siku 30 mfululizo bila malipo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana
kama Simu Dokta, Dk. Meshack Shimwela ambaye ni Bingwa wa magonjwa ya
binadamu (Physician), alisema upatikanaji
wa taarifa sahihi za kiafya ni moja kati ya hatua muhimu za kupambana na magonjwa mbalimbali.
Dk.
Shimwela alisema huduma hiyo itatoa mchango mkubwa katika kuuhabarisha
umma juu ya masuala muhimu ya kiafya na kuongeza kuwa ujumbe wa mara kwa
mara utawakumbusha watu na namna
ya kujikinga pamoja na kuchukua hatua sahihi juu ya magonjwa.
Aidha Dk.
Shimwela aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuzindua huduma hiyo kwa
ajili ya umma na kusema kuwa ‘’ Inaendana na malengo ya milenia hasa
namba sita linalosisitiza kupambana na
magonjwa mbalimbali, akiwataka Watanzania kuitumia huduma hiyo ambayo ni muhimu kwa kila mtu’’.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania ,
Kelvin Twissa alisema taarifa hizo zitakuwa katika mfumo wa ujumbe mfupi
wa maneno (sms) na mteja atakuwa
akizipata kila siku kupitia simu yake ya mkononi bure kwa mwezi baada ya kujisajili kwa kutuma neno DAKTARI kwenda 15542.
‘’Lengo la
huduma hii ni kuchochea na kusaidia wananchi kujua mambo mbalimbali ya
kiafya ambayo wamekuwa hawayajui au kuwa na taarifa zisizo sahihi,
taarifa hizo zitakuwa zikiandaliwa na madaktari
bingwa nchini wa magonjwa mbalimbali ambao wamejitolea kuelimisha
jamii, pamoja na kusaidia ustawi wa jamii kwa kuwa na jamii yenye uelewa
mkubwa wa mambo ya afya na kusaidia kuokoa maisha ya
watu wengi,’’ alisema Twissa.
Hii
itakuwa ni huduma ya kwanza ya aina yake kutolewa na Vodacom
ikiwahusisha madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kwa kutoa taarifa
kila siku za kuwasaidia kujiepusha na maradhi au kutoa
ahueni kwa magonjwa yanayowasumbua.
Madaktari
hao bingwa ni pamoja na Dk. Meshack Shimwela (Bingwa wa magonjwa ya
mwili wa binadamu (Physician). Dk. Sulende Kobhoja (Bingwa wa watoto na
moyo (Paediatricia & Cardiologist), Dk.
Munawara Kaguta (Bingwa magonjwa ya wanawake/wajawazito (OBST/Gynecologist).
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
-----
JINSI YA KUJIUNGA
0 maoni:
Post a Comment