CCM MUFINDI YACHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA VIJANA

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa
Wawakilishi wa vijana wakisoma risala
Mtaturu akikabidhiwa mkasi kwa ajili ya kukata utepe

Na Mathias Canal, Mufindi

Chama cha Mapunduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa kimeendelea na adhma yake ya kusaidia vijana katika shughuli za maendeleo Jimboni humo hususani katika kilimo na ufugaji ili kutekeleza ilani ya chama.

Katika ziara ya kuimarisha chama Wilayani humo iliyofanyika mwishoni mwa wiki, baadhi ya vijana wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji walikiomba Chama hicho kuwasaidia maeneo ya kufanyia kazi zao pasipo kusumbuliwa ili iwe nyenzo ya kujikwamua katika wimbi la umasikini.

Miraji Mtaturu ambaye ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo aliwapatia shilingi 200,000 na ahadi ya jezi pea 1 na mpira 1 na kuwataka vijana hao kujihusisha na mambo ya michezo kama njia ya kutojihusisha na wizi, ngono zembe na matumizi ya madawa ya kulevya.

Mtaturu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na vijana hao Kijijini Ihongole na kuongeza kuwa vijana ni rasilimali kubwa ya Taifa, hivyo kwa kuthamini nguvu kazi zao CCM haiwezi kuwa mbali nao kwa kuwa ni chama cha Ukombozi wa uhuru wa haki kwa watanzania.

Katika ziara hiyo kijijini hapo Mtaturu pia alifungua tawi la Wakereketwa huku vijana 40 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliamua kujiunga na CCM pamoja na zoezi la kukabidhiwa kadi na kuwa wanachama halali.

Aidha aliwaahidi vijana hao kulifikisha ombi lao walilopendekeza juu ya Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahomoud Mgimwa kuwa mlezi wa tawi hilo ili kujenga ufanisi wa kuendeleza yale ambayo amekuwa akiyatekeleza Jimboni humo.

Akioangea na Mjengwablog mmoja wa vijana ambaye alifahamika kwa jina moja la Steven, alisema kuwa CCM ni chama pekee Wilaya Mufindi ambacho hakitateteleka kwa udi na uvumba.

Sambamba na hayo Mtaturu hakusita kuzungumzia jinsi ambavyo vijana wa CHADEMA wamekuwa wakiwalalamikia baadhi ya vijana wa mtaa wa Stendi kwa kuondoa bendera za chama hicho kinyume na utaratibu huku akisema kuwa jambo hilo amekwisha litolea taarifa polisi.

"Serikali imetenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwenye daraja ambalo limekuwa likisumbua wakati wa mvua hivyo daraja hilo litajengwa katika mwaka huu wa fedha" Alisema Mtaturu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment