Filikunjombe anena kuhusu PAC


Ukweli ni kwamba sisi PAC (Kamati ya Hesabu za Serikali), tulipokuwa tunapitia hesabu za Mamlaka ya Bandari zilizoishia mwezi June mwaka 2012, tulishtushwa na matumizi makubwa ya TPA kwa mwaka ule wa fedha.

Kwa mfano, tulikuta kwa mwaka mmoja, kwenye item moja ya Master Workers Council TPA walitumia Tshs 9.6 billion.

Sisi tuliona hizo ni fedha nyingi mno kutumika kwa mkutano pekee. Hao ni Sisi PAC.
Lakini pia tulibaini kuwa TPA mwaka ule mpaka June 2012 TPA walitumia Tshs. 6.4 kwaajili ya matangazo.

Sisi tuliona hizo ni fedha nyingi mno - kutumika na taasisi kama TPA kwaajili ya matangazo kwa mwaka mmoja.

Lakini pia tulibaini kwamba kwa mwaka ULE mmoja TPA walitumia Tshs. 10 billioni kwaajili ya safari za nje na za ndani.

Sisi PAC tuliona fedha hizo ni nyingi mno kutumika kwaajili ya safari tu - kwa mwaka mmoja - na taasisi moja kama ya TPA.

Hao ni Sisi PAC.

Hatua tulizozichukua ni pamoja na kumwomba CAG afanye ukaguzi maalum kwenye matumizi hayo, ili kuondoa hiyo "sintofahamu".

We demanded for a 'value for money audit' for the above expenditures.

Ninachoweza kusema ni kwamba CAG amekwisha kamilisha uchunguzi wake. Ripoti tunayo. Ameshatukabidhi PAC. Na wao Bandari pia wamekabidhiwa.

Ninacho waombeni nyie wenzangu ni kwamba tunakutana na Bandari tarehe 15 November 2014, Sisi tukiwa tumeshaipitia ripoti na wao wanakuja kujibu maswali Yetu.

Tupeni muda. Tutawajuza ukweli wake. Kwa SASA tusiwahukumu TPA wacha tuipitie kwanza ripoti ya CAG.

Deo Filikunjombe,
Makamu Mkiti - PAC.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment