Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso anasema ameirejesha katiba nchini.
Liteni Kanali Isaac Zida alisema hayo mbele ya waandishi wa habari.Jeshi lilinyakua madaraka majuma mawili yaliyopita baada ya ghasia kupinga mpango wa Rais Blaise Compaore wa kutaka kubadilisha katiba ili aendelee kuongoza nchi, ingawa alikuwa ameshaiongoza Burkina Faso kwa miaka 27.
Hatimae alijiuzulu.
Siku ya Alhamisi viongozi wa jeshi, upinzani na mashirika ya kijamii walikubaliana juu ya utawala wa mpito, utaoongoza nchi hadi uchaguzi utaofanywa mwaka ujao.
0 maoni:
Post a Comment