Serikali ya ufalme wa Morocco itakutana na maafisa wa shirikisho la soka barani Afrika,CAF kwa ajili ya kufanya uamuzi kuhusu kuahirisha fainali za kombe la mataifa ya Afrika au la kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola katika nchi za Afrika magharibi.
Morocco imesema haiko tayari kuandaa mashindano hayo kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo.
CAF inataka michuano hiyo ifanyike kama ilivyopangwa ifikapo mwezi Januari na Februari mwakani.
Hata hivyo imeomba nchi nyingine saba kama wataridhia kuwa waandaaji mbadala,lakini mpaka sasa hakuna hata nchi moja iliyojibu ombi hilo.
Morocco ilipendekeza michuano iahirishwe mpaka mwezi Juni mwakani.
0 maoni:
Post a Comment