India na Pakistani zimeahirisha sherehe za kijeshi katika mpaka wa Wagah baada ya watu kadhaa kuuawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga.
Inaelezwa kuwa hii ni mara ya kwanza kuahirishwa kwa sherehe hizo ambazo zimekua jadi yao tangu nchi hizo mbili zilipopigana vita mwaka 1971.
Bomu lililipuka karibu na kituo cha ukaguzi upande wa Pakistani na kusababisha vifo vya watu takriban 55 na kujeruhi wengine wengi.
Wanamgambo wa Taliban walio Pakistani wamekiri kuhusika na shambulio hilo, huku wanamgambo wengine wawili wakieleza kuwa wametekeleza shambulio hilo.
Eneo la mpaka wa Wagah ni muhimu sana, watu wengi hukusanyika kila situ kutazama shughuli za kushusha bendera wakati mpaka unapofungwa.
Maafisa nchini India wamesema vikosi vya usalama mpakani vimekubali ombi la Pakistani kuahirisha sherehe kwa siku tatu ili kuruhusu shughuli za maombolezo kufanyika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment