Kumefanyika maadhimisho ya kuwakumbuka watu walipoteza uhai wao kwenye ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH17, nchini Uholanzi,ambapo maua na mishumaa ipatayo mia mbili na tisini na nane vilinavyo wakilisha idadi ya abiria waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo kabla ya ajali ambavyo viliwekwa na wanafunzi,ndege hiyo ilipopotelea Mashariki mwa Ukraine yapata miezi minne iliyopita.
Mfalme na malkia wa Uholanzi na mabalozi wa nje waliomo nchini humo walihudhuria hafla hiyo,ambapo majina ya walikufa katika ajali hiyo yalitajwa.
Ikiwa imetimia miezi minne leo, sababu za ajali hiyo mpaka sasa hazijajulikana,ingawa kikundi cha kigaidi cha Urusi kinashukiwa kuidungua ndege hiyo,ambayo ilikuwa ikifanya safari zake kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur Malaysia.
inasemekana ndege hiyo ilidunguliwa kwa kombora, na mara moja serikali mjini Moscow imekanusha taarifa hizo.
0 maoni:
Post a Comment