Matokeo ya awali Catalonia

 

Kura ya maoni Catalonia 
 
Matokeo ya kura ya maoni isiyokuwa na makubaliano iliyopigwa jana kutaka ama kutotaka jimbo la Catalonia lililoko kaskazini mashariki mwa Hispania kutaka kujitenga yanaonesha zaidi ya asilimia themanini ya wapiga kura wamepigia kura kujitenga kwa eneo hilo, huku kukiwa tayari asilimia tisini ya kura zimehesabiwa.
Kura hiyo ya maoni imelenga kutathmini idadi ya watu wanaotaka Catalonia kuwa nchi huru.Mapema kiongozi wa Catalonia Artur Mas ameelezea zoezi hilo la upigaji kura kama ni mafanikio.
Hata hivyo serikali ya Hispania imesema kura hiyo ni ya bure na haiathiri chochote.Waziri wa Sheria wa nchi Rafael Catala hiyo amesema zoezi hilo halikuwa la kidempokrasia na kulielezea kama lisilo na mafanikio yoyote na lisilofaa.
Zoezi hilo la upigaji kura limefanyika baada ya mahakama ya katiba nchini Hispania kuamuru kufanyika kwa kura hiyo ya maoni.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment