Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati |
WAKATI kilio cha vijana na wanawake nchini kikiendelea kuongezeka kutokanana kukosekana kwa fedha za kuwawezesha kujiajiri katika sekta zisizo rasmi ,huku serikali ikitenga fedha asilimia tano kila Halmashauri ya wilaya kwa ajili yao ,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alipua bomu bungeni kwa kuibana serikali.
Wakati mbunge kabati akilipua bomu hilo kwa kuihoji serikali juu ya mkakati wa kuwawezesha vijana na wanawake kujiajiri katika sekta zisizorasmi kwa kupewa mikopo na serikali kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua kali ya kuwakufuka kazi wakurugenzi wote wa Halmashauri ambao wametafuna fedha za vijana na wanawake katika Halmashauri zao.
Wabunge hao wametoa madai hayo leo wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akiulizwa swali lake la msingi kuhusiana na vijana na wanawake nchini kujiwezesha.
Katika swali hilo mbunge Kabati alitaka kujua iwapo serikali kama ina mkakati wowote wa kuwawezesha vijana ili kujiajiri wenyewe katika sekta zisizo rasmi.
"Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la vijana wanaohitimu masomo yao kukosa nafasi za ajira nchini , Je serikali inamkakati gani kuona vijana hao wanajiajiri kwa mfumo usio rasmi na kuwezeshwa .... swali la pili serikali ina mpango gani wa kuongeza elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya ufundi hasa kwa kutoa uwezo wa vyuo vya veta na shrika la Sido ili vijana wengi waweze kujiajiri wenyewe " alihoji mbunge Kabati .
Akijibu swali hilo naibu waziri wa Kazi na Ajira Gaundensia Kabaka mbali ya kumpongeza mbunge Kabati kwa jitihada zake za kuwapigania vijana bado alisema kuwa serikali toka mwanzo imekuwa ikiendesha Programu mbali mbali ambapo kwa sasa wizara yake imeandaa fedha kupitia benk ya CRDB ili kuweza kuwakopesha vijana hao ambao watakuwa wamejiunga katika vikundi ili kuweza kukopesheka na kuwaajili wenzao watakaohitaji .
Alisema kuwa ili kwa sasa wanasubiri kupata fedha hiyo ambayo kiasi hakukitaja ili programu hiyo kuanza nchini ila alisema kuwa kuwa ajira ina wadau wengi bado alitaka wadau wengine wakiwemo wabunge kuweza kutumia fursa zilizopo ili kuweza kusaidia kupunguza adha ya ajira nchini
" Swali la pili kuhusiana na VETA mheshimiwa naibu spika Veta imeanza mkakati wa kuwawezesha vijana ambao wamejiajiri wenyewe wakiwemo vijana na mamalishe kwa kuwaongezea ujuzi zaidi na tayari mikoa mmne nchini wameanza mpango wa kutoa mafunzo hayo kwa kuwapa vyeti wahitimu ..."
Mbunge Kangi Lugola |
Kutokana na majibu ya naibu waziri huyo mbunge Kigola alilazimika kuomba mwongozo na kueleza kutorizishwa na majibu ya naibu waziri juu ya maswali hayo nyeti yanayohusu mstakabari wa vijana na wanawake nchini.
" Mheshimiwa naibu spika kwanza nimpongeze mbunge Kabati kwa maswali yake ila nasikitika majibu yaliyotolewa na waziri ...mheshimiwa waziri amesema kuwa tayari inayomipango mbali mbali ya kuwawezesha vijana .....mheshimiwa naibu spika kwanini nimeomba mwongozo wako uzoefu nilioupata kupitia kamati yetu ya serikali za mitaaunaonyesha kwamba kuna mpango mzuri ambao serikali yetu iliuanzisha kuhakikisha kila Halmashauri ya wilaya hapa nchini inapata fedha za vijana na wanawake"
Kigola alisema kuwa kote walikopita fedha ambazo serikali ilitoa kwa ajili ya vijana na wanawake wakurugenzi wamekula na hazijulikani zilipo na vijana wakiendelea kukosa mikopo hivyo anamwomba Rais kuweza kuwachukulia hatua wakurugenzi hao kwa kuwafukuza kazi kutokana na hujuma waliyoifanya
"Hivi kwanini mheshimiwa Rais badala ya kuendelea kulalamika juu ya watendaji wabovu sasa kuweza kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi watendaji hao ambao wamekula fedha za vijana na ajira hakuna badala ya vijana kuendelea kulalamika huku fedha zao zikiwa vimeliwa na wakurugenzi hao mheshimiwa naibu spika naomba mwongozo wako kwanini serikali isiwakamate wakurugenzi hawa na wote wanafahamika "
Kwa upande wake naibu spika Job Ndungai alisema kuwa madai hayo ya ameyapokea ili kuona ni namnagani atang'ong'ona na serikali na kuwa wakati mwafaka watarejea kuona suala hilo linafanyiwa vipi .
0 maoni:
Post a Comment