Miaka 25 ya ukuta wa Berlin

 
 maadhimisho ya miaka 25 ya ukuta wa Berlin 

Nchini Ujerumani, maelfu ya maputo yang'aayo yaliwekwa kwenye mstari wenye urefu wa kilomita kumi na tano za uliokuwa ukuta wa Berlin na kuachiliwa wakati wa usiku kama ishara ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kuangushwa kwa ukuta huo.
Maputo hayo yalitengeneza urefu wa mita 3.5 kutoka ardhini ili kuonesha jinsi ukuta huo ulivyokuwa mrefu ,uliojengwa mnamo mwaka 1961 ili kuwazuia watu kutoka Ujerumani ya Mashariki wasiingie Ujerumani Magharibi.
Naye kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kwamba kuanguka kwa ukuta huo wa mji wa Berlin mnamo mwaka 1989 ilikuwa ni alama tosha ya tumaini la leo,kwa nchi za zilizokuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.
Wakati huo ukuta wa Berlin ukiangushwa! Kansela huyo alikuwa akiishi Ujerumani Mashariki, na kusema kwamba kumbukumbu hiyo ya miaka 25 ni siku ya furaha Ujerumani yote,lakini pia ni siku ya kukumbuka waliofungwa ama kufa wakati walipokuwa wanajaribu kutorokea upande wa Magharibi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment