Rais wa Algeria atoka hospitalini

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika hatimaye atoka hospitalini ambako alikuwa amelazwa kwa siku mbili kutokana na ugonjwa usiojulikana
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amerudi nchini Algeria baada ya kulazwa kwa siku mbili katika hospitali moja ya Ufaransa.
Kiongozi huyo ambaye alikuwa akiuguwa kiarusi alilazwa katika hospitali hiyo ili kupata matibabu katika eneo la Grenoble siku ya alhamisi.
Sababu ya kulazwa kwake hatahivyo haijulikani.
Serikali ya Algeria haijatoa tamko lolote kuhusu swala hilo.Bouteflika mwenye umri wa miaka 77 na ambaye ameiongoza Algeria tangu mwaka 1999 amekuwa haonekani hadharani tangu achaguliwa kwa hatamu yake ya nne mnamo mwezi Aprili.
hospitali ya Grenoble kusini mashariki mwa Ufaransa ambako rais wa Algeria Bouteflika alikuwa amelazwa.
Gazeti la kijimbo nchini Ufaransa Le Dauphine Libere lilisema siku ya ijumaa kwamba kiongozi huyo alikuwa amelazwa katika chumba cha kukabiliana na ugonjwa wa moyo katika mji huo wa kusini mashariki mwa Ufaransa.
Gazeti hilo lilitangaza kuwa ghorofa moja ya hospitali hiyo ilikuwa imechukuliwa ili kuimarisha usalama wake.
Rais Bouteflika alipigania vita vya uhuru wa Algeria kutoka kwa Ufaransa mnamo mwaka 1962.Alichaguliwa kuliongoza taifa hilo kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka 90.
Uchaguzi wake wa mwaka 2014 ulikosolewa na vyama vya upinzani ,vilivyosema kwamba kulikuwa na udanganyifu na kwamba Bouteflika alikuwa hafai kuwania kutokana na kuzorota kwa afya yake.
Bouteflika alipelekwa Hospitalini mjini Paris mwaka 2005 kutokana na tatizo la vidonda tumbo swala lililozua wasiwasi kuhusu afya yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment