Meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku, akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani, siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira nchini uliofanyika katika kijiji cha Tulya wilaya ya Iramba. Kulia mwenye miwani ni mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.
Na Nathaniel Limu, Iramba
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA),linatarajia kutumia zaidi ya shilingi 396 milioni kugharamia utekelezaji wa mradi wa usafi mashuleni na mazingira kwa ujumla,katika shule saba ba kata saba za wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la WaterAid Tanzania. Hayo yamesemwa na meneja wa SEMA,Ivo Manyanku, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa siku ya kunawa mikono duniani,siku ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingirav nchini, iliyofanyika katika kijiji cha Tulya wilayani Iramba.
Alitaja baadhi ya malengo ya mradi huo, kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi na jamii kwa jumla namna bora ya kunawa mikono.
0 maoni:
Post a Comment