Na Owen Mwandumbya, Lusaka Zambia
Rais
wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Anne Makinda leo tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza
ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa
aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa
maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka,
Zambia.
Katika
ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine wa
Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda, Spika wa
Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la Malawi Mhe.
Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da Piedade Dias
dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick Matibini.
Kutoka
secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, katibu Mkuu wa Bunge Bunge la
SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha
sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka, Zambia.
Kwa
mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa hiyo
Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika leo tarehe 10 Novemba,
2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona ya dunia
pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa watakaoziwakilisha nchi zao
kabla ya kufanyika kwa mazishi yake ambayo yamepangwa kufanyika siku ya
Jumanne tarehe 11 Novemba, 2014 mjini Lusaka.
Sata
aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014 jijini
Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake kilitokea
siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi
hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi yaliyokuwa
yakimsumbua.
Mwanasiasa
huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza
chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye
alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party
Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.
Sata
ambaye alibatizwa jina la “King Cobra” na wafuasi wake wakati
alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na
mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na
upinzania.
Makinda
na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada kushiriki
pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014.
0 maoni:
Post a Comment