Waziri Nyalandu alitoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kitaifa uliowashirikisha viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na wadau wa maendeleo kuhusu kujadili namna ya kudhibiti uharibifu dhidi ya rasilimali za nchi zikiwamo wanyama na misitu, juzi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Waziri Nyalandu, kukithiri kwa vitendo hivyo kunachangiwa na madai ya kuongezeka kwa soko haramu la rasilimali za nchi zikiwamo nyara za serikali katika nchi za Vietnam, Japan, Korea, China na Thailand.
Alisema matukio ya ujangili nchini hadi kufikia juzi, yameendelea kupungua kwani ni takribani miezi minne hadi sasa hakujaripotiwa matukio makubwa ya vitendo hivyo.
Aliwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria zikiwamo aina ya gobore, kuzisalimisha haraka kwa hiari, vinginevyo watakumbwa na operesheni ya nyumba kwa nyumba na kuwalazimu wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa mujibu wa Nyalandu, iwapo wananchi wanaomiliki silaha hizo wakizisalimisha kwa hiari na kukiri juu ya uovu waliokuwa wanaufanya dhidi ya rasilimali hizo za nchi vikiwamo vitendo vya ujangili, hawatachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aliongeza kuwa zoezi hilo la kwanza likimalizika itafuata hatua ya pili ya kusaka nyumba kwa nyumba kwa wale ambao hawakutii agizo la hiari na hivyo wengine kushtukizwa hata usiku wa manane.
CHANZO: NIPASHE
0 maoni:
Post a Comment