Baada ya miezi kadhaa ya utulivu katika eneo la mashariki mwa DRC, ghasia zimerejea tena.
Zaidi ya watu 120 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa kwa mapanga na mashoka mwezi uliopita katika eneo la mpakani na Uganda.
Inadhaniwa kuwa kundi la waasi kutoka nchini Uganda la ADF ndilo linalohusika na mashambulizi hayo.
Vikosi cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimekuwa kikilalamikiwa katika mji huo wa Beni kwa kushindwa kuzuia mauaji, licha ya mamia ya wanajeshi wake kuweka kambi katika eneo hilo.
Hata hivyo wenyewe wanasema ni vigumu kuweza kuwalinda raia wote, licha ya kuchukua hatua kadhaa.
0 maoni:
Post a Comment