WANANCHI IRINGA WAASWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudensiana Kisaka akizungumza na waandishi wa  habari ofisini kwake

Na Mathis canal, Iringa

Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya wilaya Iringa, Pudensiana Kisaka, amewaomba wananchi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la mpigakura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake huku akiwataka wananchi kushiriki vyema kujiandikisha ikiwa ni pamoja na kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanayemtaka kwa manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Kisaka alisema kuwa Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri za vijiji na wenyeviji wa vitingoji katika Mamlaka za Wilaya za mwaka 2014, wapiga kura wataandikishwa katika vitongoji husika kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi 29/11/2014, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika majengo la umma au maeneo ambayo msimamizi wa uchaguzi atakuwa amekubaliana na vyama vya siasa.

Alizitaja sifa za mpiga kura kuwa anatakiwa awe raia wa Tanzania, awe na umri wa mika 18 au zaidi, awe mkazi wa eneo husika lakini pia asiwe na ugonjwa wa akili.

Aidha alisema kuwa kuhusu wakazi wenye umri wa miaka 21 au zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Kijiji, ujumbe wa Halmashauri ya kijiji na uenyekiti wa kitongoji wachukue fomu za kugombea zitakazopatikana kwenye ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014.

Alisema uteuzi utafanyika tarehe 24/11/2014 ambapo fomu za uteuzi wa mgombea zitabandikwa mahali pa matangazo ya uchaguzi katika Vijiji na Vitongoji huku akisema kuwa pingamizi dhidi ya uteuzi zitapokelea kuanzia tarehe 26/11/2014 na kushughulikia pingamizi hilo hadi tarehe 27/11/2014.

Kisaka alisema kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina jumla ya wananchi 25,432 hivyo kwa maana ya uchaguzi wa serikali za mitaa idadi itategemea na wananchi waliojiandikisha kupiga kura kwa kufuata kanuni na miongozo iliyopo.

Kisaka alitoa wito kwa wananchi kujitokeza na kujiandikisha kwenye vituo ambavyo vitakuwa kwenye vitongoji vyao ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kupiga kura.

"Kujiandikisha ni jambo moja lakini la zaidi ninaomba viongozi wa vyama vya siasa kuwashawishi wanachama wao kwa ajili ya kujiandikisha kwa wingi ili wawe na haki ya kuchagua viongozi wanao wataka, lakini pia nitoe wito kwa viongozi wa siasa kuwashawishi wanachama wao kuwa watulivu wakati wa kampeni na hatimaye kukamilisha zoezi hilo salama wakati wa uchaguzi" Alisema Kisaka
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment