Wasafisha madirisha wawili mjini New York wanabahati ya kipekee kuepuka kifo baada ya jukwaa walilolitumia kusimama kuvunjika,na kuwaacha wakining'nia ghorofa ya sitini na tisa juu ya mji wa Manhattan ya chini.
Wanaume hao wawili wote ni wasafisha madirisha ya majengo marefu nchini humo,na jukwaa hilo lilipokuwa likikatika walikuwa wamejihami na vifaa vya usalama.
Baada ya taarifa za jukwaa lao kukatika na wao kubaki wakining'inia kusambaa, walikuja okolewa na kitengo cha zimamoto baada ya kukata tundu kwenye mojawapo ya madirisha ya ghorofa ya sitini na tisa.
Maafisa wa Jengo hilo la One World Trade Centre wameeleza kuwa wanahisi jukwaa hilo lilikuwa na matatizo ya kiufundi.
Jengo hilo lina urefu wa mita zaidi ya miatano na arobaini na ndilo jengo refu zaidi nchini Marekani.
0 maoni:
Post a Comment