WAZIRI NKAMIA AFUNGA MASHINDANO LUKUVI CUP

Naibu Waziri Juma Nkamia akikabidhi zawadi ya kombe

Na Mathias Canal, Iringa

Hatimaye Mashindano ya Lukuvi Cup Kata ya Migori yamemalizika kwa timu ya Mtera Shooting kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa kuilaza timu ya Home Boys kwa jumla ya goli 4 kwa 1.

Katika mchezo huo uliozikutanisha timu hizi pinzani japo zinatoka katika kata moja, hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika kila timu ikiibuka na goli moja, hivyo kupelekea mwamuzi kuamuru kuingia katika hatua ya matuta ili kupata msindi.

Ilikuwa ni timu ya Mtera Shooting iliyokuwa ya kwanza kupata goli lililofungwa na Mtei Mlimbwa katika dakika ya 86 ya mchezo kabla ya Frank jackson mchezaji wa Home boys kuisawazishia timu yake katika dakika ya 87.

Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.

Nkamia alimkabidhi mshindi wa kwanza kombe na fedha taslimu shilingi 1,000,000, ambapo mshindi wa pili alikabidhiwa kombe na shilingi 500,000, huku mshindi wa tatu akiambulia shilingi 250,000.

Alisema kuwa lengo la mashindano hayo limetimia ambapo vijana wengi walihamasika kushiriki katika michezo tofauti na dhana potofu ya vijana kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na ngono zembe.

Nkamia aliwaahidi wachezaji hao kuongea na mbunge wa Jimbo hilo ili timu bingwa iweze kwenda kondoa kwa ajili ya mechi ya kirafiki sambamba na timu kutoka Kondoa kuja kucheza katika uwanja wa Migori.

Aliwataka wadau wa michezo Mkoani iringa kuwekeza kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuisaidia timu ya Lipuli ili iweze kupita hatua ya ligi daraja la kwanza na kucheza ligi kuu Tanzania bara.

"Ni zaidi ya milioni 30 ambazo Mh Lukuvi amewekeza kwa ajili ya michezo Jimbo la Isimani, naamini lengo la mashindano haya sio kuwaomba vijana kwa ajili ya kumpigia kura bali ni kukamilisha adhma yake katika kuhakikisha vijana wana kuwa na afya bora ikiwa ni pamoja na kujiajiri" Alisema Nkamia

Hata hivyo Mashindano hayo yanatarajia kuendelea hivi karibuni ambapo itakuwa ni hatua ya Tarafa na timu itakayoibuka na ushindi wa Tarafa itajipatia Pawatila la kisasa kwa ajili ya kujiimarisha kwenye kilimo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment