Miaka 13 baada ya majengo ya awali ya kituo cha Biashara cha kimataifa WTO kuhalibiwa katika shambulio la kigaidi la Septembar 11,2001 ,kituo hicho kilichopo jijini New York kimefunguliwa kwa shughuli za biashara.
Waajiriwa katika kampuni kubwa ya uchapishaji wa Conde Nast wameanza kuingia katika jengo hilo la One World Trade Centre lenye urefu wa ghorofa 104
Jengo hilo lenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda wa miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.
Limekodishwa kwa asilimia 60% na taasisi ya serikali ya Marekani ya utawala wa Huduma imeingia mkataba wa kuchukua eneo la futi la mraba 275,000
"Mwonekano wa zamani wa jijini New York umerejea tena" Anasema patrick Foye mkulugenzi mtendaji wa mamlaka ya Bandari ,ambayo yanamiliki eneo hilo lililolejeshewa hali yake
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment