Katibu Mkuu wa Chama, Dk. Willibroad Slaa amekitaka CCM kujiandaa kisaikolojia ili kikabidhi dola kwa amani baada ya uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka huu kwa sababu chama hicho hakiwezi kuchaguliwa tena na wananchi. Akihutubia umati mkubwa wa maelfu ya wananchi wa Sumbawanga waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ndau, Katibu Mkuu amesema kuwa sera, mipango na mikakati ya CCM imeshindwa badala yake chama hicho kimeongeza maadui wa taifa kutoka watatu wa awali yaani umaskini, ujinga na maradhi na sasa wameongeza wengine wabaya zaidi; rushwa na ufisadi wa kutisha ambao unaliangamiza taifa. Akirejea ripoti mbalimbali za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambazo zimekuwa zikionesha ufisadi wa kutisha huku kukiwa na udhaifu wa serikali katika kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika, Katibu Mkuu amefafanua ripoti hizo na kuzielezea kulingana na mazingira husika ya wananchi wa Sumbawanga (all politics is local) wanaokabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma muhimu. Katibu Mkuu Dk. Slaa ameendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao wanayoishi ili wajiandikishe kwa ajili ya kupiga kura Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, akisisitiza kuwa hiyo ndiyo fimbo ya mnyonge baada ya kudharauliwa na watawala walioweka pamba masikio na kukumbatia ufisadi kwa miaka mitano wakisahau dhamana waliyopewa uchaguzi mkuu uliopita. Attached: MAANDAMAKUSINDIKIZA (1).jpg (6.55 MB) Reply Kurugenzi ya Habari 20:58 Yesterday Baada ya mkutano, wananchi wakampatia heshima...hawakumwacha aende peke yake hotelini. Reply Regina1 21:00 Yesterday Kwa kweli itabidi wajiandae kisaikolojia Huu umati unatisha Watu wamejawa furaha tele Octoberrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr rrrrrrrrrrrrrrrrrr peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee eeeeeeeeeeee Reply SIDANGANYIKI2015 21:03 Yesterday Teh teh teh ni shida,Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa Binadamu mchungu,dr.Silaha alikimbia wakati tume inatoa matokeo ya urais mwaka 2010. Reply SIDANGANYIKI2015 21:04 Yesterday Ajiandae kisaikolojia kukimbia kwenda kujificha tena huyo! Reply OKW BOBAN SUNZU 21:04 Yesterday CCM hata aibu hawana,wengine mawaziri wanataka kupewa urais kwa hoja za wapinzani Reply SIDANGANYIKI2015 21:06 Yesterday By Regina1: Kwa kweli itabidi wajiandae kisaikolojia Huu umati unatisha Watu wamejawa furaha tele Octoberrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr rrrrrrrrrrrrrrrrrr peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee eeeeeeeeeeee umati sio dili go and ask Hon.Mrema he knows the secreat behind the scene in 1995 sio huyo mzee wetu! Reply songera 21:06 Yesterday Ameongea kama nani.hata yeye anapaswa kujiandaa kushindwa vibaya mno Reply SIDANGANYIKI2015 21:08 Yesterday By OKW BOBAN SUNZU: CCM hata aibu hawana,wengine mawaziri wanataka kupewa urais kwa hoja za wapinzani raha chezea Ikulu,la sivyo UKAWA wasingejoin the move to state house na wataishia soko la feri kununua fish! Reply swissme 21:09 Yesterday Huyu jamaa anapendwa sana na Watanzania. swissme Reply SIDANGANYIKI2015 21:13 Yesterday By songera: Ameongea kama nani.hata yeye anapaswa kujiandaa kushindwa vibaya mno By swissme: Huyu jamaa anapendwa sana na Watanzania. swissme Usijidanganye ndugu wanamzuga tu kwani si ndo huyu alisimama 2010 miaka 5 iliyopita akiwa na nguvunzaidi ya leo na ule mkono ulikua haujapindana na kushindwa ku work sasa leo ana jipya gani na ni watz hao hao walimchinjia baharini! Reply Kurugenzi ya Habari 21:13 Yesterday Heshima ya wananchi kwa kiongozi wao... Attached: MAANDAMAKUSINDIKIZA (2).jpg (5.64 MB) Reply Jile79 21:15 Yesterday Naweza kusema ccm wakiwa wapinzani Itabidi wasubiri sn...... ccm=chama cha majambazi Reply SIDANGANYIKI2015 21:19 Yesterday By Jile79: Naweza kusema ccm wakiwa wapinzani Itabidi wasubiri sn......ccm=chama cha majambazi Wewe unawaza hivyo wakati na wao CCM wanafanya kila mbinu CDM iendelee kusubiri milele! Reply SIDANGANYIKI2015 21:20 Yesterday By Kurugenzi ya Habari: Heshima ya wananchi kwa kiongozi wao... Huo ndo ukarimu wa watanzania kwa wageni hasa maeneo ya bara sio jambo geni Tanzania! Reply Kurugenzi ya Habari 21:21 Yesterday Reply hazole1 21:23 Yesterday hilo gwanda ambalo nilimuona amevaa mwaka 2010 na ndio nimemuona amevaa leo 2015 na hajawahi kubadilisha inamaana bado yuko vitani kuiokomboa tanzania kutoka kwa adui mkubwa ccm na huyo mzee lazima awe rais kwasababu amepata kibari moja kwa moja kutoka kwa mungu Reply Mwakaboko King 21:25 Yesterday By kurugenzi ya habari: mie simo nasubiri hiyo oktoba 2015 wasipolizwa na ccm tena hawa maana imewapania sana hawa! Reply Mwakaboko King 21:28 Yesterday By hazole1: hilo gwanda ambalo nilimuona amevaa mwaka 2010 na ndio nimemuona amevaa leo 2015 na hajawahi kubadilisha inamaana bado yuko vitani kuiokomboa tanzania kutoka adui mkubwa ccm na huyo mzee lazima awe rais kwasababu amepata kibari moja kwa moja kutoka kwa mungu Mkuu uwe makini Mungu anaanza na herufi kubwa la sivyo ni mungu mdogo asiye na mamlaka. Reply omunga 21:28 Yesterday Mwaka wa ukawa huu Reply Page 1 of 10 1 23 ... Last Up Copyright JamiiForums.com
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment