MWAKYEMBE AKANUSHA KUDILI NA LOWASSA

kupitia JICHOPEMBUZI  Mwakyembe akanusha taarifa iiyokuwa inasambazwa kuwa atadili na Lowassa Mapengo 17 08:25 Today Kupit Mwakyembe amekanusha vikali tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwake kwamba ameapa kudili na Edward Lowassa katika sakata la Richmond. Amesema amekwisha kamilisha hatua za awali za kutoa taaria katika mamalaka zinazohusiaka ikiwemo Polisi Makao Makuu Kitengo cha Cyber Crime, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kubaini mtandao huo ambao ulianza harakati zake tangu Lowassa atangaze nia. "Sio uungwana kuchezea majina ya watu wanakosa ujasiri wa kuelezea hisia zao hadi watumie majina ya watu wengine, mtandao huo nauona kuwa ni hatari" Amesema huenda kwasababu ya joto la uchaguzi suala hilo nipo katika msukumo wa kisiasa huku akitaka hatua kali ziweze kuchukuliwa. Ameapa kudili na kundi hilo "Nimedhamiria kukomesha tabia hii, nimekwenda Polisi Kitengo cha Cyber Crime (Mkosa ya Jinai ya Mtandao) na TCRA, kulalamikia mchezo huu hatari wa kihuni na tayari vyombo hivi vimeanzisha uchunguzi huu mkali, ili kubaini wahusika wote wanaoandaa hizo taarifa na kuzituma kwenye sehemu mbalimbli na wanaozituma sehemu nyingine hizo taarifa, lakini lazima tupeleke ujumbe ulio wazi kwasababu nchi yetu inaendeshwa kwa misingi ya sheria" Hata hivyo, amesema kundi hilo lilianza polepole, na Tanzania Daima amelitaja kuwa lilikuwa mbele sana kwa kuandika habari kuwa "Mwakyembe na Sitta Kujibu Mapigo" na waliandika bila kunihoji. Amesema baada ya kupata taarifa hizo aliingia kwenye Mtandao Maarufu nchini wa JamiiForums.com unaoendesha mijadala kwa jamii. Taarifa hizo aliziona kwenye blogs nyingi akakuta habari hizo lakini cha kushangaza ni pale alipoona taarifa hiyo Mwanahalisi Online kwamba amesema atapambana kufa na kupona ili Lowassa asiingie Ikulu. Sasa hawa Mwanahalisi sijawahi kuongea nao ikifuatiwa na taarifa nyingine kuwa nimesema Lowassa hana sifa. Reply stanlthecreator 08:28 Today Ameanza kuogopa nguvu za Mungu,Lowasa ni Mpango wa Mungu Reply idawa 08:31 Today By stanlthecreator: Ameanza kuogopa nguvu za Mungu,Lowasa ni Mpango wa Mungu Mungu yupi huyo.? Reply patriotic crusader 08:32 Today Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hahusiki kwa namna yoyote na matamko yaliyoonekana kwenye magazeti ya Tanzania daima, Mwanahalisionline na mtandao wa jamiiforums dhidi ya Edward Lowassa na ameripoti suala hilo polisi na TCRA kwa hatua zaidi. Source: Clouds fm Reply Kagalala 08:33 Today By stanlthecreator: Ameanza kuogopa nguvu za Mungu,Lowasa ni Mpango wa Mungu Kuna Miungu wengi, hata mashetani wana Mungu wao. Reply Chachu Ombara 08:34 Today Kasoma wakati kaamua atulie. Reply umla 08:35 Today By stanlthecreator: Ameanza kuogopa nguvu za Mungu,Lowasa ni Mpango wa Mungu msimuingize Mungu kwenye upuuzi wenu....sema anaogopa nguvu ya pesa sio Mungu. Reply Sikonge 08:35 Today Pasco hebu njoo huku. Naona Makongoro njia inakuwa nyeupe.... Reply Mr Suggestion 08:36 Today Imemchukuwa siku ngapi kukanusha huu uvumi? Huyu Dr anazeeka vibaya sana Reply Salary Slip 08:37 Today Wanasiasa si watu wa kuaminika hasa walio madarakani.Mwanasiasa anaweza kuikana hata kauli yake mwenyewe kutegemena na upepo wa kisiasa unavyovuma akilenga kulinda maslahi yake binafsi na ya chama chake. Kwahiyo msishangae kuona jambo hili linaisha kimya kimya bila kusikia habari ya Polisi wala TCRA. Reply TUJITEGEMEE 08:37 Today Mbona muda umepita sana tangu ianze kusambazwa hiyo taarifa! Alikuwa anasubiri nini kuikanusha? Au Clouds "wamefoji kanusho"? Reply Abdulwahid 08:40 Today mhh haya wanasiasa hao Reply Feedback 08:44 Today Huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono, kaanza Mwakyembe kukana maneno yake mwenyewe bado Nape anaangalia upepo. Reply Pasco 09:08 Today By patriotic crusader: Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hahusiki kwa namna yoyote na matamko yaliyoonekana kwenye magazeti ya Tanzania daima, Mwanahalisionline na mtandao wa jamiiforums dhidi ya Edward Lowassa na ameripoti suala hilo polisi na TCRA kwa hatua zaidi. Source: Clouds fm Kufuatia kuripoti Polisi, ngoja na mimi niwahi fasta fasta kulifuta bandiko langu hili Ushauri wa Bure Kwa Hon Dr. Harison Mwakyembe Pasco Reply Up Copyright JamiiForums.com

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment