Home
Advertise With Us
Home HABARI MOTOMOTO SIMBA
MESSI NA SIMBA SC ‘NGOMA DROO’ TFF, WARUDISHWA MSIMBAZI KUJADILI MKATABA MPYA WA 2015/2016, HUU WA SASA…
Mahmoud Zubeiry 6/09/2015 05:09:00 PM HABARI MOTOMOTO , SIMBA
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Simba SC kuketi na mchezaji wake, Ramadhani Yahya (pichani kulia) Singano ‘Messi’ kujadili namna ya kuingia Mkataba mpya, baada ya pande zote kuafiki Mkataba wa sasa una hitilafu.
Katika kikao cha leo, makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Simba SC iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati yake ya Utendaji, Collins Frisch wakati Messi aliandamana na Mussa Kisoky wa Chama cha Wanasoka Tanzania (SPUTANZA).
“Katika kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC,”amesema Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
Katibu huyo wa zamani wa Yanga SC, ameongeza kwamba kwa pamoja pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya kwa ajili ya Mkataba utakaoanza msimu mpya wa 2015/2016.
Aidha, Mwesigwa amesema TFF inazitaka klabu nchini kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba na wachezaji, makocha na waajiri wengine.
“TFF inao mkataba mama ambao klabu zote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao. Aidha TFF inawataka wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi,”amesema Mwesigwa.
Katibu huyo ameongeza kwamba, TFF itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya pande zote mbili, wachezaji na klabu.
Barua ya hukumu ya kesi ya Messi na Simba SC leo
Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo kwamba imeghushi Mkataba wake.
Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika mwakani.
Na Messi si mchezaji wa kwanza kuishutumu Simba SC kughushi Mkataba wake, kwani wachezaji wengine za zamani wa klabu hiyo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Kevin Yondan wamewahi kutoa malalamiko kama hayo wakati wanahamia kwa mahasimu, Yanga SC.
Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus
About Mahmoud Zubeiry
Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
RELATED POSTS
MRUNDI 'WALIYEMKOSAKOSA' SIMBA NA Y...
OKWI ‘AWAUMBUA’ YANGA SC, ASEMA SIM...
SIMBA SC YAMUAMBIA MESSI; "DAWA YAK...
Post a Comment
Older Post Home
MISIMAMO LIGI MBALIMBALI
Home
MSIMAMO LA LIGA- HISPANIA
MSIMAMO LIGI KUU- ENGLAND
MSIMAMO BUNDESLIGA- UJERUMANI
MSIMAMO SERIE A- ITALIA
MSIMAMO LIGUE 1- UFARANSA
MSIMAMO LIGI KUU YA VODACOM- TANZANIA
RATIBA MICHUANO MBALIMBALI DUNIANI WIKI HII
MATOKEO MICHUANO MBALIMBALI DUNIANI WIKI HII
FUATILIA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI ZINAZOENDELEA HIVI SASA DUNIANI
ANGALIA AZAM TV HAPA
Home
KWA WANAOTUMIA KOMPYUTA BONYEZA HAPA
KWA WANAOTUMIA SIMU ZA MKONONI BONYEZA HAPA
MDHAMINI WETU
LIKE PAGE YETU FACEBOOK
ZILIZOSOMWA ZAIDI WIKI HII
MAVUGO TAYARI SIMBA SC, NI MALI YA MSIMBAZI KWA MIAKA MIWILI IJAYO
Mchezaji bora wake mpira; Mavugo anakuja SImba SC Na Princess Asia, DAR ES SALAAM SIMBA SC imekaribia kabisa kukamilisha usajili wa mc...
OKWI ‘AWAUMBUA’ YANGA SC, ASEMA SIMBA SC NDIYO MPANGO MZIMA
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM TANGU jana usiku kumekuwa na uvumi ambao chanzo chake haswa hakijulikani- kwamba mshambuliaji wa kimat...
IDADI YA WACHEZAJI WA KIGENI LIGI KUU KUONGEZWA HADI SABA
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM IDADI ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaweza kupanda hadi saba kuanzia ...
FC PLATINUM ‘KIROHO SWAAFI’ YABARIKI NGOMA KUTUA YANGA SC
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM FC Platinum ya Zimbabwe imesema kwamba wapo kwenye mazungumzo na Yanga SC ya Tanzania juu ya biashara ya ...
MFARANSA ALIYEIPELEKA NUSU FAINALI AFRIKA COTTON SPORT ATAJWA SIMBA
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM KOCHA Mfaransa, Didier Gomez de Roza ametajwa kuwa ndiye anayekuja kufundisha Simba SC, lakini Mwenyekit...
PITIA TOVUTI NYINGINE
Sport | Mail Online
Rangers face years in Celtic shadows as the finance gap widens between Old Firm rivals - Chairman Dave King has been warned it could take him five years to bridge the gap between Rangers and Celtic - and longer if his vow to spend big this summ...
22 minutes ago
MICHUZI BLOG
EALA SPEAKER AND SOMALIA PARLIAMENT COUNTERPART HOLD TALKS IN KAMPALA - *The Speaker of the Federal Parliament of Somalia, Rt. Hon Mohamed Osman Jawari leafs through the EALA Strategic Plan as the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel ...
24 minutes ago
FUFA: Federation of Uganda Football Associations
INTERNATIONAL BUILD UP: Uganda 1-1 Gambia - Uganda 1-1 Gambia | 61’ Robert Sentongo, 73′ Omar Jagne Detailed Report coming soon
44 minutes ago
Futaa.com
Deche hattrick shoots down Strikers - Dennis Kombora Deche scored a hat trick to enable Fair Deal Furniture shoot down Bokole Strickers 5-0 in the FKF Mombasa Premier League match played at Bom...
50 minutes ago
saluti5
MANCHESTER UNITED YAHUSISHWA TENA NA USAJILI WA RAHEEM STERLING, NICOLAS GAITAN NA DANI ALVES - Manchester United imeripotiwa kukamilisha mipango ya kuwanasa kwa mpigo Raheem Sterling, Nicolas Gaitan na Dani Alves. Mashetani hao Wekundu wamedhamiria ...
16 hours ago
IDADI YA WASOMAJI
38806170
GOOGLE+ FOLLOWERS
Copyright © 2015 BIN ZUBEIRY
Designed by 2jiachie
Created By Sora Templates and My Blogger Themes
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment