JICHOPEMBUZI Tuesday, July 28, 2015
Kada mkongwe wa CCM Ambaye Alikuwa Waziri Katika Serikali ya Mwl. Nyerere Atimkia CHADEMA Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi na ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Nazar Nyoni (84), amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Nyoni ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na maneno ya wabunge waliomaliza muda wao, Tundu Lissu na Halima Mdee. Alikuwa akizungumza mbele ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini, wanachama na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea ubunge na udiwani wa Jimbo la Morogoro Mjini.
Nyoni alisema licha ya kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kiongozi serikalini tangu mwaka 1975 hadi 1994 huku akiwa na kadi mbili ya Tanu na CCM, amemua kujiunga na Chadema pia baada ya kufuatilia mambo mengi ya msingi ikiwamo Bunge la Katiba na Bunge na kutambua kuwa chama kimoja chenye umoja na mbinu moja ni Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa).
"CCM kwa sasa imechoka na kubaki kula fedha za nchi na kwa msingi huo, nikiwa mzee, nimeamua kuhamia Ukawa ili niseme kabla sijaaga dunia kuwa hakuna chama kinachoweza kuongoza Tanzana kwa sasa zaidi ya Chadema ama Ukawa," alisema Nyoni. Awali, mtia wa kugombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chadema, Marcos Mgweno, aliwaasa wana-Morogoro kuukataa unyonge walionao kwa sasa kwa kuichagua Chadema kwa ajili ya maendeleo yao.
Mgweno alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri duniani lakini utajiri huo hauwanifaishi wananchi husika bali wachache kwa manufaa yao binafsi.
Naye Katibu wa Chadema Wilaya Morogoro Mjini, Esther Tawele, aliwataka wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla, kutambua kuwa hatma ya maisha yao ipo mikononi mwao hivyo ni nafasi yao kutumia Ukawa katika kuwaletea mabadilko.
JICHOPEMBUZI blog Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana ) ‹ › Home View web version
0 maoni:
Post a Comment