▼ Jumatano, 29 Julai 2015 KWANINI CHADEMA WAMEMCHUKUA LOWASSA??
Mnamo mwezi February mwaka huu Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliingia ubia na kampuni maarufu duniani inayojihusisha na tafiti za siasa (Political Research) ijulikanayo kama Greenberg Quinlan Rosner. ( www.gqrr.com/ ).
UKAWA walitaka kujua kama wana nafasi ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu. Kampuni hiyo ilimaliza utafiti wake mwezi May mwaka huu na haya ndio yalikua majibu; 1. Ikiwa CCM itamsimamisha Lowassa kugombea Urais, na UKAWA wakamsimamisha Dr.Slaa, CCM watashinda kwa 58% dhidi ya 42% za UKAWA. 2. Ikiwa CCM itamsimamisha mgombea mwingine asiye Lowassa kushindana na Dr.Slaa, CCM itashinda kwa 54% dhidi ya 46% za UKAWA. 3.
Ikiwa UKAWA itamsimamisha mgombea mwingine ambaye si Dr.Slaa na CCM ikamsimamisha Lowassa, CCM itashinda kwa 68% dhidi ya 32% za UKAWA.
4. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mtu mwingine ambaye sio Dr.Slaa na CCM ikamsimamisha mtu mwingine ambaye sio Lowassa CCM itashinda kwa 57% dhidi ya 43% UKAWA.
5. Ikiwa watu wote wa CCM wanaotaka Urais wakiwekwa Pamoja na wa UKAWA wakawekwa pamoja kisha wapigiwe kura za Urais kama wagombea huru, Lowassa ataongoza kwa 14% kisha Dr.Slaa atafuata kwa 09%, Membe 04% na wengine chini ya hapo.
6. Ikiwa Lowassa atagombea kupitia UKAWA atapunguza kura za UKAWA kwa 06% lakini ataziongeza kwa 24%. Hii ina maana kuwa katika watu 100 wa CHADEMA watu 6 hawataipigia kura CHADEMA kwa sababu hawamtaki Lowassa.
Lakini Lowassa ataleta watu wapya 24. Yani CHADEMA itapoteza kura 6 za wanachama wake lakini itapata kura mpya 24 mpya. DATA ANALYSIS Ukisoma vzr huo utafiti hapo juu utagundua kuwa Lowassa anaongeza umaarufu wa CCM kwa 18%. Kwa hiyo kuondoka kwa Lowassa kutaipunguzia nguvu CCM kwa 18%. Sasa ikiwa CCM yenye Lowassa ina nguvu 58% na UKAWA yenye Dr.Slaa ina nguvu 42%, maana yake ni kwamba umuondoa Lowassa CCM ni kupunguza nguvu yao kwa 18% yani (58-18) = 40%. Na kumleta Lowassa UKAWA ni kupunguza nguvu ya UKAWA kwa 6% lakini kuongeza kwa 24%. Kwa hiyo chukua 42 toa 06 kisha jumlisha 24 utapata 60%. Sasa jumlisha 40% za CCM na 60% za UKAWA kama haiji 100%?? Kwa hiyo UKAWA yenye Lowassa inashinda uchaguzi kwa nguvu kubwa zaidi kuliko ambavyo CCM ingeshinda ikiwa na Lowassa. Na hii ni kwa sababu ujio wa Lowassa utaivunja CCM vipande vipande. Na ili uweze kuishinda CCM lazima uivunje vipande kwanza. Huwezi kuishinda CCM ikiwa imesimama imara.
Nchini Kenya KANU ilishindwa kirahisi baada ya kuvunjwa vipande, Zambia UNIP ilishindwa baada ya kuvunjwa vipande, na nchi nyingine za Afrika vivyo hivyo. Na njia rahisi ya kukivunja chama tawala ni kwa kuondoa watu wenye ushawishi ktk chama hicho. Fredrick Chiluba alikua mtu mwenye ushawishi mkubwa akiwa UNIP lakini alipoondoka kwenda MMD huo ndio ukawa mwisho wa UNIP maana alikua na ushawishi na aliondoka na kundi kubwa la watu. Nchini Kenya akina Najib Balala, George Saitoti, Musalia Mudavadi, Raila Odinga, Mwai Kibaki etc walikua watu wenye ushawishi sana ndani ya KANU.
Lakini walipoondoka kwenda NARC hiyo ndio ikawa mauti ya KANU. Hii ni kwa sababu watu hawa walipoondoka, waliondoka na kundi kubwa la wafuasi. Hivyo basi hata Lowassa atasaidia kuivunja CCM na hatimaye kuiwezesha UKAWA kushinda kirahisi. Ikumbukwe Nyerere aliwahi kusema huwezi kuishinda CCM imara yenye umoja.
Kwa hiyo njia rahisi ya uishinda CCM ni kuivunja vunja vipande. Na tayari kazi hiyo imeanza rasmi. BAADA YA UTAFITI. Baada ya ripoti ya utafiti huo wa GNR mnamo mwezi May, UKAWA walikaa na kutafuta njia ya kufanya. Walijua wazi CCM ikimpitisha Lowassa UKAWA itaangushwa hata imsimamishe nani. Na laiti CCM wangeona ripoti ya utafiti huo wasingefanya kosa la kumkata Lowassa. Wangempitisha ili waishinde UKAWA kirahisi.
Kwa hiyo UKAWA walikua wanafuatilia sana mchakato wa CCM huku wakiomba usiku na mchana wasimpitishe Lowassa. Na kweli Mungu akajibu maombi yao. Lakini UKAWA wakatafakari ikiwa watamsimamisha Dr.Slaa kushindana na Magufuli bado UKAWA itashindwa kwa kupata 46% dhidi ya 54% za CCM kama utafiti unavyoonesha. Kwa hiyo ili kuishinda CCM ni kufanya nini? Ili kuishinda CCM ni kumshawishi Lowassa ajiunge na chama kimojawapo kinachounda UKAWA ili apewe nafasi ya kugombea na kuiwezesha UKAWA kushinda. Na ndivyo ilivyotokea. Kwa hiyo kwa mujibu wa utafiti huo UKAWA itashinda kwa 60% na CCM 40% kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sasa nani asiyetaka ushindi? Siasa ni hesabu, siasa ni namba, siasa ni sayansi. Kama hujui hesabu usifanye siasa. at 12:37 AM Shiriki Hakuna maoni: Chapisha Maoni Links to this post Unda Kiungo ‹ › Nyumbani Ona toleo la wavuti Inaendeshwa na Blogger.
0 maoni:
Post a Comment