WALIOUA SIMBA MAARUFU KUSIMAMA KIZIMBANI

▼ Jumatano, 29 Julai 2015 WALIOUA SIMBA MAARUFU

KUSIMAMA KIZIMBANI Watu wawili watapandishwa kizimbani leo nchini Zimbabwe kujibu mashtaka ya kumuua simba aliyepewa jina la Cecil.

Hata hivyo, daktari wa meno kutoka Marekani Walter James Palmer aliyemuua simba huyo aliyekuwa maarufu zaidi nchini Zimbabwe hayumo miongoni mwa washtakiwa hao. Palmer na wenzake waliingia mbugani usiku ambapo walifunga mzoga wa mnyama kwenye gari lao kumvutia Cecil atoke mafichoni na awafuate na ndipo Palmer alipomuua.

Kwa mujibu wa shirika moja lislilo la kiserikali linalotetea uhifadhi wa wanyama, Cecil alikatwa kichwa na kuchunwa ngozi na mpaka sasa haijulikani kichwa chake kilipo. Palmer alikuwa amelipa dola 50,000 kupata kibali cha kuwinda.

Amesema aliwategemea wenyeji wake kumwelekeza wanyama wapi wanaoruhusiwa kuwindwa na kwamba hakufahamu kuwa Cecil alikuwa mnyama aliyependwa na hakutakiwa kuwindwa.

at 3:19 AM Shiriki Hakuna maoni: Chapisha Maoni Links to this post Unda Kiungo ‹ › Nyumbani Ona toleo la wavuti Inaendeshwa na Blogger.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment