Bashir Aenda China Bila Kuogopa Kukamatwa na ICC


Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim Ghandour, amesema mashtaka dhidi ya  Rais Omar al Bashir, wa Sudan, yaliyowasilishwa mbele ya  mahakama ya uhalifu wa  kimataifa ya ICC huko The Hagiue ni tuhuma za nchi za  ulaya pekee.
Bwana Ghandour, amesema mashtaka hayo yanapingwa na  na jumuia nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na viongozi wa umoja wa Afrika.
Waziri huyo alizungumza hayo kabla ya Rais Omar al Bashir kuelekea Beijing, China, kuanza ziara ya siku nne nchini China.
Akizungumza na sauti ya Amerika kwa njia ya simu, waziri Ghandour, amesema kuwa Rais Bashir, anendelea kutembelea nchi mbali mbali anazoalikwa na viongozi wenzake  bila hofu ya kukamatwa.
Rais Bashir, Jumatatu ameanza ziara ya siku nne huko China chini ya mualiko wa serikali ya China kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya kushindwa kwa Japan katika vita ya pili vya dunia.
Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo wa Sudan kutembelea China. Waziri Ghandour, amesema kwamba Sudan na China zina uhusiano mzuri.
Ameongeza kusema, Sudan, ni miongoni mwa mataifa ya juu barani Afrika yenye ushirikiano mkubwa wa kiuchumi na China, na nchi hiyo iliisaidia Khartoum wakati wa kipindi kizito cha historia yake pale Marekani ilipoitenga.
Amesema ziara ya Rais Bashir, itakua ni pamoja na mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, mkutano na wafanyabiashara wa China waliowekeza Sudan pamoja na watu kutoka Sudan wanoishi China.
Rais Bashir, alishitakiwa mwaka 2010 kwa uahlifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na vita ya jimbo la Darfur.
China haikutia saini mkataba wa kuundwa  ICC lakini ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

from Blogger http://ift.tt/1Kowz4F
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment