Misri yaanda uchaguzi wa bunge


Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Ayman Abbas, anasema uchaguzi utaanza October 18 na kumalizika baada ya awamu mbili ya siku mbili, hapo November 23.
Rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi

Rais wa Misri Abdel Fattah el SissiMisri inapanga kufanya uchaguzi wa bunge ambao umecheleweshwa kwa muda  hapo mwezi October na November mwaka huu. Hiyo ni  zaidi ya miaka mitatu ya bila kuwepo na bunge. Wachambuzi wanasema bunge jipya huwenda likarudisha baadhi ya uaminifu wa kimataifa, lakini hio huwenda lisiweze kusaidia maisha ya watu wa huko Misri.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Ayman Abbas, anasema uchaguzi utaanza October 18 na kumalizika baada ya  awamu mbili  ya siku mbili, hapo November 23.
Abbass anaonya wagombea ubunge, dhidi ya kuchochea ghasia, au kujaribu kufanya wizi wa kura.
Bunge hilo jipya litafanya serikali kuonekana kuwa halali zaidi kwa wawekezaji wa kimataifa, anasema Said Sadek mwanasoshologia wa kisiasa. Anasema kukiwa na zaidi ya vyama mia moja vya kisiasa, na kanuni  nyingi mpya, huwenda ikachukuwa muda mrefu kabla kupatikana mafanikio makubwa.
Sadek anasema bunge ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Misri. Lina wabunge 596. Anasema Misri hiajawahi kuwa na bunge kubwa kama hilo.
Kwa sasa, sheria Misri zinapitishwa na rais Abdel Fattah el Sissi, ikiwa ni pamoja na sheria mpya dhidi ya ugaidi iliyopitishwa wiki mbili zilizopita, na ambayo imevutia ukosowaji kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadam, ambayo yanasema, sheria hiyo itatumiwa kuwanyamazisha wapinzani, na vyombo vya habari.
Misri imekuwa bila ya bunge tangu June mwaka 2012, pale bunge lililotawaliwa na kundi la Muslim Brotherhood lilipovunjwa. Uchaguzi unaokuja ulicheleweshwa kutoka March kwa sababu za kiufundi na kisheria.
Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanasema sababu ya kweli kwa uchelewesho huo ni kuwa serikali inaweza kulishinda kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood, na kuhakikisha wafuasi wao hawashindi viti katika bunge jipya.

from Blogger http://ift.tt/1Q5mTL6
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment