NA HII YA MWANAUME KUSAMBAZA UGONJWA KWA MAKUSUDI ISIKUPITE MTU WANGU!!!!!

JICHOPEMBUZI Na hii ya mwanaume kusambaza ugonjwa kwa makusudi isikupite mtu wangu!!!

Nimekutana na stori kutoka Iceland inayomhusu mwanaume mmoja kutoka Nigeria ambaye amekamatwa na polisi kwa madai ya kusambaza ugonjwa wa UKIMWI kwa makusudi.

Mwanaume huyo ambaye jina lake bado halijajulikana ni raia kutoka Nigeria ambaye amekuwa akijaribu kupata uraia wa sehemu hiyo toka mwaka 2014.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka  kituo cha police cha Iceland, Iceland Review Report imesema:

>>>“sehemu kubwa ya upelelezi tunaoufanya sasa hivi ni kujua kama wanawake wengine wamekutana kimwili na huyu mwanaume zaidi ya ile idadi tulionayo kwenye ripoti zetu…”<<< Iceland Police.

>>>“taarifa zingine za matukio ya kiualifu ya mwanaume huyu bado zinakusanywa.

Kwa sasa shitaka kubwa dhidi yake ni kujihusisha na vitendo vya kimapenzi kwa nia ya kusambabza ugonjwa wa UKIMWI- kitendo ambacho kikithibitishwa kitakuwa ni kinyume na sheria zetu za nchi”. <<< Iceland Police.

 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment