Nilimnunua xxxx Nikamtambulisha Nyumbani Kwa Wazazi, Utata Ukatokea..!!!

“Unata nife ndo uoe? Nataka kuwaona wajukuu zangu”Ni kauli alioitamka baba yangu mzazi Siku moja alipokuja kunitembelea, iliniuma sana.

Nadhani hata nyie mnalifahamu suala la kuoa au kuolewa ni mipango ya mtu mwenyewe pale mda wake utakapofika atafanya maamuzi yake mwenyewe hii ni kutokana na mtu kujipanga kwake.

Ni muda mrefu wazazi wananisumbua nioe na mimi bado sijampata mwanamke ninaemtaka,nikaona ili niwaridhishe wazazi nikaona ngoja niwapake mafuta kwa mgongo wa chupa.

Nikachukua maamuzi nikaenda sehemu zile wanazojiuza wadada wale wa High quality nikamchagua mmoja mzuri sana nikamueleza nia na dhumuni langu tukakubaliana nimlipe kwa dau flani niende nae kama mpenzi wangu na awe na nidhamu zote kwa wazee.

Basi nilifanikiwa na walifurahi sana tafrija fupi ikapita Mara wanandugu wakaitwa njooni mmuone mchumba wa flani kila mmoja alimpenda huku nikiambiwa umechagua kifaa.

Niliona kama maigizo flani ambayo mbeleni pataishia pabaya na kweli ikawa hivyo.Sasa nimeletewa taarifa kwamba ndugu wamekaa kikao wameshapanga kila kitu kuhusu suala la harusi hadi tarehe.Nimechanganyikiwa vya kutosha na yule kahaba kachapa zake kona

Nipeni mawazo jamani nifanye nini?


from Blogger http://ift.tt/1hCPPij
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment