Babu Seya na Mwanawe Wakiwa Chini ya Ulinzi wa Magereza |
Kuna watu wanajaribu kupotosha nini hasa mantiki ya Mgombea Edward Lowassa kuahidi kushughulikia suala la Sheikhs wa Zanzibar na suala la Babu Seya.
Suala la Sheikhs wa Zanzibar liliihusisha Chadema kabla hata Lowassa hajahamia huku. Binafsi niliombwa na Dr Slaa kulishughulikia, lakini bahati mbaya nilikuwa nina cases kadhaa zilizonifanya nikwame. Lakini cha muhimu zaidi ni kwamba wana Wakili, tena Wakili mahiri tu na ambaye ni Mwanachama wa Chadema. Amepambana sana, na anaendelea mpaka leo.
Issue yao ni complicated, na ni mfano tu wa issues zinazo athiri haki za wananchi kwa kukosekana tu utashi sahihi wa kisheria na kiutawala.
Mojawapo wa pertinent issues ni mgogoro wa iwapo wanatakiwa kishtakiwa Bara, au Zanzibar inakosemekana walitenda huo ugaidi.
Na kuna masuala ya Sheiks wale kulalamika kutendewa kinyume wakiwa chini ya ulinzi.
Kuna suala pia la ucheleweshaji wa upelelezi, hata kama tuna-assume case dhidi yao ina mashiko.
Asiyefahamu anaweza kudharau uzito wake, lakini ni suala linaloleta hisia kali kwa sehemu ya waumini wa kiislamu.
Lowassa atakuwa Rais wa ajabu kama vision yake ya kisheria haitajumuisha suala pertinent kama hilo. Huwezi jadili general concepts bila kuchagua specifics kadhaa kama mfano.
Pia, Lowassa hajasema atamtoa Babu Seya kwa stroke ya pen on a whim. Wala hajasema hiyo ni priority yake above all else kwa upande wa sheria. Alichosema within the limited confines za muda ni kwamba serikali yake itakuwa makini sana na masuala ya utawala wa sheria. Issue ya Babu Seya na hao Sheiks ni representation tu ya matatizo yaliyopo. Na malalamiko yaliyopo. Issue ya Lawrence Masha na wale vijana 19 wa 4U Movement tuliowapigania juzi, imepigia mstari.
Pamoja na kwamba ni suala linalogawa opinion, ni naivety kujidai eti issue ya Babu Seya si moja ya issues zinazoleta mjadala wa kisheria na kihisia mpaka leo hii. Suala la ni namna gani linashughulikiwa, ni suala la ushauri wa kisheria kutoka kwa wataalamu wa Rais Lowassa (kipindi hicho).
from Blogger http://ift.tt/1Ewjjsv
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment