Waalimu walalamikia kutolipawa mapesa yao

WADAU wa elimu na baadhi ya walimu
mkoa wa Njombe wamesema kuwa kama serikali haita timiza matakwa yao watafanya
mabadiliko mwaka huu hasa kwa kurekebisha mishahara kwa walio panda madaraja.
Hayo yamebainishwa, Mkoani Njombe,
wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa
wa Njombe, ambapo kwa jimbo la Njombe kuna mgombea Emmanuel Masonga, wadau hao
walisema kuwa watafanya mabadiliko kama serikali itaendelea kuto wajali.
Mmoja wa walimu walio hudhuria
katika mkutano huo na kusikia sera ya elimu inayo nadiwa na Chadema, Frances Manga,
alisema kuwa serikali kama haita walipa ongezeko la mshahara  kwa walimu waliopanda madaraja mwezi wa mai
mwaka huu na kuwa kwa mkoa wa Njombe hasa halmashauri ya mji huo kunawaalimu
wanapandisha madaraja wakiwa na  miaka
mitano kazini tofauti na sera ya ajira ya taifa.
Alisema kuwa mwisho wa mwezi
ulio pita kama katika mishahara yao hakuta onekana ongezeo lolote la mshahara
watafanya mabadiliko ili kuitoa serikali ya chama cha Mapinduzi kwa maana
kimewakandamiza vyakutosha.
Alisema kuwa walimu wakekuwa
hawaonekani kama wanamuhimu kwa taifa hili kwa kuwa maombi yao hayatekelezwi
kwa wakati na kusema kuwa kuna mgomo wa chini chini katika mashule hapa nchini.
Mwalimu Manga alisema kuwa
wamekuwa wakidai pesa zao kwa mda mrefu na mamlaka zinazo husika kama Halmashauri
na TSD wanapigiana mipira na kuw awameahidiwa mwisho wa mwezi Agosti watapatiwa
pesa zao na kupewa barua ambazo zinaonyesha wamepandishwa madaraja tangu mwezi
Mai mwaka huu.
Mgombea ubunge, Emmanuel Masonga Aidha akiwa jukwaa Mgombea
ubunge kwa Chadema jimbo la Njombe kusini Emmanuel Masonga (Pichani) alisema kuwa sera za
Chadema ikishiga dola kutakuwa na ufuatiliaji wa hali ya juu masuala ya elimu.
Alisema kuwa sera ya chama
chao taifa inasema kuwa kipaumbele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu
ni elimu.
Alisema akiingia bungeni
atahakikisha kuwa walimu na sekta zingine watu hawalalamiki kwa kupunjwa
mishahara amba kwa kuonewa na waajili kwa kuwa watakuw awakiyapokea matatizo
yao moja kwa moja na kuyawasilisha serikalini hasa kwa kuwa watakuwa na makao
yao kwa wananchi.  

“Mimi nitakapo kuwa mbunge itakapo kuwa elimu bure
nitasaidia elimu kuboresha katika sekta ya umma na sio katika sekta binafsi na
ubura kuikomboa njombe,” alisema masonga.


Alisema kuwa bila kuwapo kwa elimu
hakuna kilimo chenye tija na kuwa elimu itasaidia kuinua kilimo, alisema kuwa
kila mwisho wa bajeti ya Tanzania kumekuwa na mswada wa sheria ya fedha lakini Wabunge
wamekuwa hawapati uwakilishi wa ukweli kuwatetea na kuleta uwiano wa kikodi wa
pembejeo za kilimo ili wakulima kulima.

from Blogger http://ift.tt/1LNkAOj
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment