Kerry azungumzia kitisho cha wa wanamgambo wa IS na Iran



Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amekuwa na mazungumzo na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif juu ya kitisho  cha wanamgambo walio na  itikadi kali wa dola la kiislamu nchini Iraq na Syria, mazungumzo yaliofanyika mjini New York Marekani. Mawaziri hao wawili walikutana kwa zaidi ya saa moja jana katika hoteli moja mjini humo na kuzungumzia hatua zilizopigwa katika majadiliano, juu ya nyuklia na pia kuzungumzia kitisho cha wanamgambo wa ISIL. Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani, amesema Iran ina mchango wa kutoa   wakati Marekani ikitafuta kuunda muungano wa kupambana na wapiganaji wa jihadi wanaodhibiti sehemu kadhaa nchini Iraq na Syria.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment