Watu 42 wakiwemo watoto wauwawa nchini Syria.

Shirika la kutetea haki za binaadamu nchini Syria limesema, mashambulizi ya angani yaliofanywa na serikali ya Syria katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi, yamesababisha mauaji ya watu 42 wakiwemo watoto 16 katika mkoa wa Idlib Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Shirika hilo lililo na makao yake nchini Uingereza limesema mashambulizi ya angani yaliofanywa siku ya jumapili mchana na jioni yaliwauwa watu 19 wakiwemo watoto sita nje ya mji wa Saraqeb, na watu wengine 23 wakiwemo watoto kumi, wakauwawa katika mji wa Ehsim. Mkoa huo upo chini ya udhibiti wa waasi nje ya mji wake mkuu Idlib. Shirika hilo limesema idadi ya waliouwawa inatarajiwa kuongezeka kutokana na wengi kuwa mahututi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment