Wanaume wa jamii hiyo
waliohusika katika tukio hilo, waliwatanguliza wanawake na watoto waliolala barabarani ili kuzuia magari yasipite, wao (wanaume) wakiwa na fimbo, mikuki na mapanga walifuata nyuma wakiamrisha magari yote ya wabunge, likiwemo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, yasimame.
Hata hivyo, askari polisi pamoja na maofisa usalama waliokuwa wakiongoza msafara huo uliokuwa ukitokea Wasso kuelekea Olduvai, walifanikiwa kuyachepushia baadhi ya magari, likiwemo la waziri, yapite upande mwingine katika pori hilo, ingawa baadhi ya magari yalilazimika kusimama baada ya kuzidiwa nguvu.
Nditiye ameongeza kuwa baada ya vikao vya Loliondo, kamati itakutana pia na viongozi wa baraza la wafugaji la Wilaya ya Ngorongoro. Akizungumzia vurugu za Arash, Waziri Maghembe amewaomba wakazi wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na watanzania kwa ujumla waiache kamati ya Bunge ifanye kazi yake.
0 maoni:
Post a Comment