Tayari Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imefungua mashimo yaliyopo Donge Chechele kwa ajili ya kazi za kuchimba mchanga baada ya shughuli hizo kusitishwa kwa wiki moja na kusababisha bei ya mchanga kupanda sambamba na bei ya matofali.
Katibu Mkuu wizara hiyo, Juma Ali Juma alisema kazi za uchotaji wa mchanga zimeanza ambapo sasa Serikali inasimamia wenyewe shughuli hizo kwa ajili ya kuona miongozo yake ya uvunaji wa rasilimali hiyo unafuatwa kwa mujibu wa sheria.
Juma alisema Serikali imeamua kusimamia kazi za uchimbaji wa mchanga kufuatia rasilimali hiyo kuanza kupungua kwa kasi kubwa. Kwa mfano, alisema sekta binafsi inayojishughulisha na kazi za miradi ya ujenzi zinahitaji zaidi ya hekta 100,000 ya mchanga ambao kwa sasa haupo tena nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na mali zisizorejesheka, Yussuf Haji Kombo alisema tayari serikali imeweka mikakati na kupiga marufuku maeneo ya kilimo kuchimbwa mchanga.
Alisema imebainika kwamba maeneo mengi ya kilimo ikiwemo mkoa wa kaskazini Unguja yameathirika na kazi za uchimbaji wa mchanga ambapo baadhi ya kilimo hivi sasa hakikubali tena na kustawi vizuri.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua kwamba bei ya matofali kwa ajili ya kazi za ujenzi imepanda wiki mbili zilizopita kutoka tofali moja sh 700 hadi kufikia 1,000.
Bei hiyo haijashuka licha ya serikali kutangaza kuanza tena kuchimbwa kwa mchanga katika mashimbo yaliyopo Donge Chechele ambapo upo uwezekano wa bei hiyo kuongezeka zaidi kutoka ilipo sasa kutokana na gharama nyingine
0 maoni:
Post a Comment