Jeshi
la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu watatu wakazi wa Matwiga wakiwa na
nyara za serikali ambazo ni vipande 9 vya meno ya tembo na mikia 2 ya twiga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo
amesema kuwa 09.03.2017 Jeshi la
Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa TANAPA wamefanya msako wa pamoja katika
Kijiji na Kata ya Lupatingatinga,Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa
kuwakamata watu watatu wakiwa na nyara za serikali.
Watuhumiwa
hao ni HUSSEIN KHAMIS [33] ,ISSA MLAWI [31] na ZACHARIA MUSA [36].
Watuhumiwa
ni majangili.
Upelelezi
unaendelea na mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani.
Katika
tukio la pili Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Mamlaka ya Chakula
na Dawa [TFDA] limefanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wawili ambao ni ERASMO DANDA [50] Mfanyabiashara na
Mkazi wa Ihanga Wilaya ya Mbarali ambaye amekamatwa akiwa na pombe kali
zilizopigwa marufuku na serikali aina ya “viroba original” boksi 99 zenye
thamani ya Tshs 9,768,000/= zikiwa
zimehifadhiwa katika stoo yake.
Mtuhumiwa
mwingine ni JOYCE BATHLOMEO [36]
Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaoni Wilayani Chunya,
NESTORY FILBERT [23] mkazi wa Lupatingatinga Wilaya ya Chunya, FILBERT KALUMANZILA [60] ,JOSHUA MWAKAJA [42] mkazi wa
Makongolosi JACKSON ELIAS [55] mkazi
wa Makongolosi Wilaya ya Chunya.
Na
katika tukio la tatu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya msako kwa
kushirikiana na maafisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tawi la Mbeya [TFDA]
katika eneo la Rujewa Kata na Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali na kufanikiwa
kumkamata mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la ASUNGUKYENI MBILINYI [45]
Mkazi wa Rujewa akiwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku na Serikali.
Vipodozi
vilivyokamatwa katika msako huo ni betasol lotion tube chupa 240, betasol cream
chupa 144, Epiederm cream tube 12, diproson cream tube 12, carlolight cream
chupa 8, cocopup chupa 20 na citrolight chupa 6.
Jumla
ya thamani ya bidhaa yote iliyokamatwa ni Tshs.
1,380,000/=.
Mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
0 maoni:
Post a Comment