MKUU wa Mkoa wa Mwanza,
John Mongela ameziagiza halmashauri zote za mkoa huo kuwa katika kipindi cha
mwezi mmoja ziwe zimenunua sio chini ya tani 20 za mbegu za mtama kwa ajili ya
kuzigawa kwa wakulima.
Alisema hayo wakati
alipokuwa akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano katika ofisi yake.
Alisema halmashauri
itakayoshindwa kutekeleza agizo hilo itachukuliwa hatua, akisisitiza kuwa
serikali haiwezi kuona wananchi wake wanahangaika na kushindwa kupata mbegu
hizo kwa wakati muafaka.
Alisema mwezi ujao mkoa
kupitia timu yake utapita kila halmashauri kukagua mashamba ya mtama ili
kujiridhisha kama agizo lake limetekelezwa kwa wakati.
Katika hatua nyingine,
Mongela alisema mkoa uko kwenye mazungumzo na kampuni za bia nchini Tanzania
Breweries na Serengeti Breweries kuona ni namna gani wanavyoweza kuwa na
mkakati wa pamoja wa kuzalisha zao la mtama.
Alisema hali hiyo inatokana
na asilimia 70 ya bidhaa zinazotumika kutengeneza bia zinatokana na zao la
mtama, ambapo asilimia 95 ya zao hilo hununuliwa kutoka nje ya mkoa wa Mwanza
wakati mkoa una uwezo wa kuzalisha zao hilo.
0 maoni:
Post a Comment