UVUVI HARAMU MAENEO YA ZIWA VICTORIA HUSUSANI MWANZA




BAADHI ya viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa wamedaiwa kuwa ni sehemu ya washiriki wa uvuvi haramu, hali iliyotajwa inasababisha ugumu katika vita dhidi ya uvuvi huo usio rafiki katika baadhi ya maeneo ya Ziwa Victoria, hususani mkoani Mwanza.



 


Hayo yalisemwa jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela wakati alipokuwa akieleza hatua zinazochukuliwa na mkoa katika kudhibiti shughuli za uvuvi haramu kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa (RCC).
Alisema uvuvi haramu unahusisha matumizi ya zana haramu za uvuvi zilizozuiliwa kisheria ambazo husababisha kuvuliwa kwa samaki wachanga, kuvua na kufanya biashara ya samaki na mazao yake bila ya kuwa na leseni ikiwemo usafirishaji wa mazao ya uvuvi ndani na nje ya nchi bila ya kulipia ushuru na mapato ya serikali.
Aliongeza kuwa, hali hiyo imesababisha idadi ya viwanda vya samaki mkoani Mwanza kupungua kutoka viwanda 12 hadi kufikia viwanda vinne vinavyofanya kazi hadi hivi sasa.
Alizitaka halmashauri zote za mkoa wa Mwanza kuweka mkazo katika kupambana na uvuvi haramu kwa maslahi mapana ya mkoa na taifa ili kuwezesha juhudi za pamoja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi mkoa wa Mwanza, John Bunyanya aliomba halmashauri ziongeze bajeti kwenye halmashauri zao kwa ajili ya kuwasaidia wavuvi wanaonyang’anywa vifaa vyao
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment