Baada ya kuwashtua watu kwa ujio wa albamu yake mpya mwezi huu, sasa Lady Jaydee ameweka wazi tarehe ya kuachia albamu hiyo.
Albamu hiyo ambayo ameipa jinala ‘Woman’ inatarajiwa kutoka 31 Machi mwaka huu kwa mujibu wa cover la picha aliloliweka kwenye mtandao wake wa Instagram.
Ndani ya Woman zinatarajiwa kusikika nyimbo kadhaa ambazo tayari zimeshasikika ikiwemo ‘NdiNdiNdi’, ‘Sawa Na Wao’ na ‘Together Remix’.
Mwezi ulipita kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, malkia huyo wa Bongo Flava aliweka wazi kuwa atafanya lauch ya albamu hiyo mwezi huu.
0 maoni:
Post a Comment