Serikali ya mkoa wa Dodoma imeingia makubaliano na kampuni ya saruji ya Dangote kuuza saruji katika ujenzi wa miji mipya ya makao makuu ya nchi (Dodoma).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini humo mara baada ya kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa kampuni za Dangote Alhaaj Saada Ladan, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema kuwa Serikali ya mkoa wa Dodoma imeipa eneo kampuni hiyo ya Dangote kama eneo la bandari kavu, ambapo saruji inayouzwa nje ya nchi, zitauziwa kutoka Dodoma.
Alhaaj Ladan kwa upande wake aliishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliotoa kwa kampuni hiyo, huku akisema kuwa ikizingatiwa hata mji wa mkuu wa Nigeria Abuja, ulijengwa na wataalamu wa kitanzania, na hivyo hawana budi nao kutoa mchango wao kuijenga Dodoma.
By: Emmy Mwaipopo
0 maoni:
Post a Comment